ALIYEKUWA mgombea nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Mara, Gabriel Mnasa Sabi ameuomba uongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Umoja wa Vijana makao makuu, kuingilia kati chaguzi za umoja ambazo zimetawaliwa na vitendo vya hujuma na rushwa.
Sabi ambaye juzi aishindwa kwa tofauti ya kura 14 dhidi ya Ditu Manko , amesema jijini Dar es salaam mara tu baada ya kutua leo asubuhi kuwa uchaguzi wao haukuwa huru na haki kwani matokeo yalijulikana kabla ya kupiga kura.
Alisema kuwa alitangaziwa matokeo hayo wakati wa kampeni kwa madai kuwa nafasi ya uenyekiti lazima itoke wilaya ya Tarime kutokana na nguvu ya kifedha.
“Hali hiyo ilinifanya kunyong’onyea hata kabla ya uchaguzi, hata hivyo nilipiga moyo konde na kuingia kwenye uchaguzi, matokeo yakawa yaleyale, nilishangazwa sana na wafuasi wangu wakaamua kutoendelea na uchaguzi huo,” alisema Sabi.
Alisema kuwa baada ya matokeo hayo, fujo zikaanza kwani wafuasi wake walichoka kuona vitendo vya uonevu vya waziwazi na kuongeza kuwa pamoja na wafuasi wake kutoka, uchaguzi huo uliendelea na kuhoji hao waliochaguliwa walipata kura hizo kwani sidhani kama idadi ya wapiga kura kwa mujibu wa katiba ilifikiwa.
“Kasoro hizi si za kuziacha kwani zinawagawa wanachama, ni lazima zikemewe kwani bado kuna chaguzi nyingi ndani ya chama,” alisema.
Alifafanua kwa kusema kuwa hana tatizo na uongozi wa juu wa CCM kutokana na sera madhubuti zenye kuleta maendeleo ya nchi, ila kilio chake ni viongozi wanaokipaka matope chama hasa wa ngazi ya chini.



Inasikitisha kuona kwamba tumeingia katika tabia ya kudai kuhujumiwa kila pale tunaposhindwa kwenye chaguzi, kama ni kweli haya mambo kwanini hawa walengwa wasichukue malalamiko yao na kupeleka kwenye vikao husika vya vyama vyao badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari ambako huhitaji kutoa ushahidi wowote.Ikibidi tumia Mahakama
ReplyDeleteHivi kwanini tabia ya kukiri kwamba tumeshindwa huwa haipo kwani hata huyu jamaa angeshinda mpinzani wake lazima angekuja na kulalamika, ingekuwa poa kama angesema mapema kwamba kuna wadau walisema mwenyekiti lazima atoke tarime na sio anasema sasa hivi
ReplyDelete