
Sheikh mkuu Wilayani Tunduru Alhaji Waziri Chilakweche akiwa hospitali

Rajab Abdalah (17)
--
Na Steven Augustino,Tunduru
Watu wanaodhaniwa kuwa ni Waislamu wenye msimamo Mkali wa Dini wamemvamia na kumpiga Shekh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilayani Tunduru Alhaji waziri Chilakweche na kumsababishia maumivu makali.
Kabla ya tukio Shekh huyo alifatwa nyumbani kwake na vijana na kumuomba watoke nae nje ya eneo la nyumba yake wakidai kuwa wanaomba awasaidie kusuluhisha Mgogoro uliokuwa umezuka katika msikiti wa Kitumbini katika Mtaa huo.
Sambamba na tukio hilo pia kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajab Abdalah (17) Amelazwa katika Hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Tunduru akiwa hajitambui baada ya kushambuliwa kwa mapanga na watu ambao walidaiwa kukimbilia katika tukio la shambulizi la Shekh Chilakwechi.
Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa manane kuamkia leo ambapo katika madai yao vijana hao walimtuhumu Alhaji Chilakwechi kuwa amekuwa akishiriki na kula vyakula vya wakirsto.
Akiongea kwa taabu Alihaji Chilakwechi alidai hakuwa na ubaya nao na wala hajwahi kugombana na mtu hali ambayo inamshangaza na anaiomba Serikali ifuate mkondo wake kwa wahusika.
Kuhusu tuhuma za yeye kushiriki katika shughuli za dini katika madhehebu ya wakristo alidai kuwa hicho siyo kitu cha ajabu kwa viongozi wa dini na kuongeza kuwa wao kama viongozi wa dini huwa na ushirikiano na huitana na kutembeleana kwa vile dini hairuhusu uhasama miongoni mwao.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Bw. Deusdedth Nsimekli amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshji la polisi linaendelea na uchunguzi ili kujua kiini cha tukio hilo.
Aidha kamanda Nsimeki alikiri pia kufahamu matukio ya udini yanayo endelea Wilayani Tunduru nakuongeza kuwa jeshi limejipanga kuhakikisha kuwa wanadhibiti vitendo hivyo.


Pole shekhe kwa yaliyokukuta. Ni hatari sana inapofika mahali waumini wako wanataka kukutoa roho.
ReplyDeleteSasa wanashambuliana wenyewe kwa wenyewe...hv jamani tunataka kuipeleka wapi nchi yetu ya Tanzania? Tutakuja kujuta hapo baadaye. Hv uongozi wa nchi umeshindwa kuthibiti hii hali jamani?
ReplyDeleteTanzania imefika pabaya. Kama serikali isipokuwa makini makubwa yanaweza tokea.
ReplyDeletekwani amekula sakramenti ya meza ya bwana?
ReplyDeletewanashambulia viongozi wao tena ma-alkhaj, watatuhurumia kweli akina sisi watu wa kitabu? Si Mungu atuhurumie tu jamani, uhusiano na Mungu ushakuwa janga
ReplyDeleteJamani hivi wagonjwa wetu wanahudumiwaje?hebu tazameni huyu mgonjwa ambaye anasemekana hajitambui,ukiona picha tu mwili wote unasisimuka,anaonekana na majeraha makubwa na drip halafu kafungwa pingu!!huu si ubinadamu ni unyama wa hali ya juu.Kwa nini wagonjwa walio katika hali mbaya au wasiojitambua labda kuhangaika kwa maumivu nk.wasipewe huduma maalum ya uangalizi wa ziada? kama hakuna staff wa kutosha basi hata ndugu au jamaa zao wawe pembeni ya vitanda vyao.Nimetokwa na machozi kuona hii picha.Hivi kazi ya uuguzi siku hizi imekuwa ya kikatili kiasi hiki?hapo kama kinatolewa chochote hata kama huumwi utapata huduma nzuri na wanaoihitaji kama huyu kijana wanaadhibiwa kwa kufungwa kamba na pingu.Mungu amponye kijana wa watu kwa miujiza na uwezo wake.
ReplyDeleteTanzania nchi yenye amani imekwenda wapi???
ReplyDeleteSasa ndo naamini kwamba hata waliochoma makanisa hawakua waislamu ila ni watu wanaotaka kuupaka matope uislamu yaani haya mambo ni kama nigeria Boko Haramu hili kundi halipo kabisaa kiongozi wao alishakufa ila ni kuna watu wanao ishui nje ya nigeria wanalipa watu kufanya fujo ili nchi isiwe na amani sasa naona Tanzania ndo tunaelekea
ReplyDeletemimi ni mwislamu na napenda nikemee vikali vitendo vya waisilamu wenye msimamo mkali kumdhuru shehe mkuu wa Tunduru, huu ni ukatili usio na msingi wowote zaidi ya ujinga, kwanza kabisa naomba niwavue heshima ya kuitwa waislam ukweli hao sio waislamu ni wahuni wa mtaani, mwisilamu wa kweli sio muhuni wa kukata mapanga binadamu mwenzake, mmelaaniwa nyinyi wahuni mnaotumia dini yetu njema ya usilamu kuvuruga amani, miaka yote dini zote Tanzania zinashirikiana hata ziwe za kienyeji kichawi, tumeishi kwa amani miaka yote,kila familia ya Kitanzania imechanganya dini zote mpaka mwaka huu 2012 kila mtanzania mwislamu ana ndugu yake wa damu ambaye ni mkristo na hivyo hivyo kwa ndugu zetu wakristo wana ndugu wa damu waislamu tunashirikiana shughuli zote iwe harusi kanisani waislamu tunaingia kanisani iwe maulid ya mtoto wakristo wanaingia msikitini leo hii nyinyi wahuni msio na kazi za kufanya mnanunuliwa na vibaraka kufanya fujo mlaaaniwe nyinyi na uzao wenu hamtafanikiwa hata siku moja kuvuruga amani ya Tanzania tunashukuru serikali kuwabaini na kuwaadhibu hao laaaana kum watanzania wenzangu tuchukue hatua ya kuwakemea wahuni hao wachache mpaka waumbuke na waache msikubali kuacha kikundi cha binadamu wachache kuharibu amani yetu
ReplyDeletekabla ya kusema chochote lazima tujue ukweli wa mambo. nashauri tupate ukweli maana tunaweza kuambiwa ni waislam wenye msimamo mkali kumbe sio kweli ila ni watu wanajitahidi kuchafua dini yetu tukufu. Inawezekana si waislam kabisa au waislam wanaotumika na wasio waislam kuuchafua uislam. Ndugu zangu tunapoenda watu watafikiri wanauchafua uislam ila likigeuka itakuwa ni aibu na kusagana meno. Namuomba Allah atuonyeshe ukweli na haki itawale kwenye kila tuhuma dhidi ya dini yako tukufu
ReplyDeleteTanzania ya leo ni kama jipu linalosubiri kupasuka! SERIKALI please chukueni hatua za haraka kabla hao wahuni wachache hawajaendelea kuleta maafa. Ni Mungu gani huyo wanayemuabudu wao ambaye hataki washirikiane na wakristo????!!!! Jamani, tuendako sipo, je hao watu wanaishi kwa kuhudumiwa na waislam tu katika huduma nyingine kama hospitali, elimu, vyakula etc. Hii inashnagaza sana, binadamu wanapokuwa wabaya kuliko wanyama!
ReplyDeletehakuna dini tukufu. Dini zote zina matatizo yake maana zote zilianzishwa na binadamu. Mungu tu ndo mtukufu!
ReplyDeleteNdugu yangu mimi naamini dini ya Uislam haijaanzishwa na binadamu, bali ni muongozo kutoka kwa Allah jinsi ya kuishi hapa duniani. Kwa kuwa unakubali kwamba Mungu ni mtukufu basi na huu muongozo(Uislamu) aliotuletea nao ni muongozo mtukufu pia.
DeleteJamani Huu Muamko wa Kidini kufikia hapa umekuwa ni tatizo!
ReplyDeleteTulishasema mara nyingi humu ya kuwa,
1.Kigezo cha Muamko wa Kidini wa kundi moja sio Kuwafanyia ubaya watu wa dini nyingine.
2.Mara zote Dini zote zinasisitiza wema na kuwa huwezi kutekeleza Dini kwa kufanya Ubaya.
Nafikiri hili ni tatizo la Kisiasa lakini linawakilishwa kwa mgongo wa kupitia kwenye Dini kitu mbacho sio sahihi.
Au pia hili ni tatizo la watu hawa kutekeleza Dini bila kuhudhuria Mafunzo ya awali ya Dini na Uumini wanajikuta wakifanya mambo bila kujua Misingi stahili ya kuyafikia.
Mtu aliyesoma Dini akaelimika hawezi kutekeleza Dini kwa Jazba na kwa njia ya ubaya.