Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni Mh. Dkt. Getrude Rwakatare akitoa Ujumbe kwa Watanzania waliohudhiria Ibada Maalum ya Kuliombea Taifa ambapo ametaka watu kutobaguana kwa misingi ya Dini, Ukabila wala Siasa na kusema pamoja na Utawala bora pia tunahitaji maombezi ili tuweze kufikia Malengo yaliyokusudiwa kulipeleka Taifa linapotakiwa kufikia.
Dkt. Rwakatare amesema nia kubwa ya kufanya Ibada hiyo ya Maombezi ni kutaka kuweka usawa kutokana na siku za hivi karibuni kuibuka kwa Matamko mbalimbali kutoka kwa watu tofauti wakiwemo viongozi wa Kitaifa, Kidini na wa baadhi ya Makundi yanayohitilafiana na kusema tukiomba kwa jina la Mungu kila kitu kitakwenda kama tulivyomuomba ili Tanzania iendelee kuwa nchi ya Amani na Utulivu kama ilivyokuwa miaka yote ambayo ni kimbilio la watu wa Mataifa mbalimbali kwa sababu Watanzania hawajui kuchukiana na wamekuwa watu wa kushikamana kwa miaka yote.
Picha Juu na Chini ni Waumini waliohudhiria Ibada Maalum ya kuliombea Taifa wakinyanyua bendera juu kuimba na kuabudu kwa furaha bila kuonyesha tofauti ya matabaka.
Tanesco na wizara ya ardhi walihudhuria??
ReplyDeleteamani hiyo inayoombwa kwa sababu side moja safi!...ndio mtasema hivyo ila upande mwingine unakandamizwa,..hakuna amani tangu kipindi cha mwl. bali hofu na woga na vitisho ndio viliwekwa, tena hata kuhoji misingi ya kugawana kwa usawa.,
ReplyDeletekwanza tuheshimiane ndio itakuwa amani ya msingi kuliko hii ya angani.
Huu ni mkutano wa kidini, bendera za Taifa za NINI?
ReplyDeleteWe anon wa 01:2200. Bendelea haina tatizo lolote na udini, ni ishara tu ya kulipenda Taifa lako, ulilozaliwa na kukulia as your mother land, ni ishara tu ya kujivunia, mahala popote pale, hata ukiwa nchi za watu na mkutano wa aina yoyote ile waweza shika bendela yako, kuonyesha watokea wapi na wajivunia Taifa lako
ReplyDeleteWe anon wa 01:2200. Acha ujinga hakuna nchi ambayo matabaka yanagawana kwa sawa keki ya Taifa, mchapa kazi ataenjoy zaidi keki ya Taifa kuliko anayeshinda kulialia na kuandamana bila kujihangaisha
ReplyDelete