Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na mratibu wa mahusiano baina ya Global Fund na Mabunge Duniani Ndg. Svend Robinson, walipokutana kabla ya kuanza kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini Quebec, Canada.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimtambulisha Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mhe. Dr. Perpetua Nderakindo Kessy kwa Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda kabla ya kuanza kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini Quebec, Canada.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifuatilia taarifa mbalimbali na maazimio ya Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 127 wa IPU Mjin Quebec, Canada. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda na Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
Mkurugenzi wa Maktaba na Utafiti wa Bunge Ndg. Kileo Nyambele anaye muwakilisha katibu wa Bunge Dkt. Thomas kashilila akishiliki kikao cha makatibu wa Mabunge yote wanachama wa Mabunge ya Dunia (IPU) katika Mkutano wa 127 wa chama hicho mjini Quebec, Canada. Kulia kwake ni Afisa dawati la IPU kutoka Tanzania Ndg. James Warbarg.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...