Mkurugenzi wa Kampuni ya kusambaza vipoza hewa (Air Condition) Unicool, Mohamed Rwenyemamu(kushoto) akimkabidhi zawadi ya kikombe na simu aina ya Sumsang Galaxy mshindi wa mashindano ya Unicool Monthly Mug kwa mwezi wa October ndugu Joseph Tairo.
===== ====== ====
TAIRO BINGWA MICHUANO
YA GOFU YA UNICOOL MONTHLY MUG
Mchezaji Joseph Tairo wa Dar Es Salaam Gymkhana ametwaa
ubingwa wa michuano ya gofu ya Unicool Monthly Mug kwa kupiga mikwaju ya net 68
kwenye uwanja wa Lugalo jijini Dar Salaam mwishoni mwa wiki.
Mashindano hayo yaliandaliwa na klabu ya Lugalo chini ya
udhamini wa kampuni ya Unicool inayojishughulisha na usambazaji wa vipoza hewa
(Air Conditions). Baada ya kushinda, Tairo alisema mashindano yalikuwa mazuri
na wachezaji wote walionyesha upinzani wa hali ya juu sana.
Nafasi ya pili katika mashindano hayo ilikwenda kwa Charles
Sanga aliyepata net 77 kwa kumshinda Mkuu wa majeshi mstaafu George Waitara kwa
c/b baada ya wote kupata net 77. Kwa upande wa wanawake mshindi alikuwa Amina Khamisi
aliyeshinda kwa mikwaju ya netti 72, nafasi ya pili ikaenda kwa Sarah Denis
aliyepata netti 73.
Kwa upande wa ‘Division A’ mshindi alikuwa Shabani Kibuna
aliyeshinda kwa netti 68, nafasi ya pili ilichukuliwa na Abdallah Yusuph
aliyepata netti 71 na ya tatu ikaenda kwa Brandy Mitchel aliyepata netti 77. Upande wa ‘Division C’ mshindi alikuwa Moses Amateku
aliyeshinda kwa netti 66, nafasi ya pili alikuwa Mohamed Rwenyemamu aliyepata
netti 71 na ya tatu akaenda kwa Ali Mfuruki aliyepata netti 72.
Mkurugenzi mtendaji wa Unicool, Mohamed Rwenyemamu alisema
kuwa kampuni yake imeridhika na idadi kubwa ya wachezaji waliojitokeza
kushiriki mashindano hayo kila mwezi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...