Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga kulia akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanza kuuzwa kwa tiketi za shindano la Taifa la Redds Miss Tz kushoto kwake ni katibu mkuu wa kamati ya Miss Tz Bosco majaliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga amesema kuwa,Kutokana
na ukubwa wa shindano kwa mwaka huu wale wote watakaofanikiwa kuingia
ukumbini watakaa katika viti maalum vilivyowekwa katika hadhi ya
kimataifa na kila tiketi itagarimu kiasi cha shilingi laki moja
(100,000) za kitanzania.
Kwa upande wa burudani kutakuwa na burudani nyingi sana na zitaongozwa nawasanii nguli hapa nchini kama Diamond Platnum,Winfrida Josephat’Rachel’s pamoja na Wanne star ngoma troupe.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...