Mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Abdallah Juma kushoto na Salim Tawfik wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu nia yao ya kujitoa kwao siku ya leo katika kesi hiyo kutokana na kile walichoita  usumbufu wanaofanyiwa wateja wao wa kuhangaishwa na kukosa kupelekwa Mahakama ya Kwerekwe kwa muda muafaka 
 Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Sheikh Farid Hadi Ahmed kushoto akiwa na wenzake sita walioletwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga wakiwa hawana ndevu na kufunguliwa mashtaka manne mapya mahakamani hapo yakiwemo kuharibu mali za watu zenye thamani ya Shl.Milioni 50 na kufanya vurugu za makusudi zakuhatarisha amani katika nchi
 Baadhi ya Askari wa kutuliza fujo wakiwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga kwa lengo la kulinda usalama na  amani Mahakamani hapo
Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO wakiwa wanatoka katika Mahakama Kuu ya Zanzibar Vuga baada ya kufunguliwa mashtaka manne mapya..Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
 
Na Mohammed Mhina, 
wa Jeshi la Polisi Zanzibar
 
VIONGOZI wanane wa makundi mawili ya Kiislamu Zanzibar wamefikishwa katika Mahakama Kuu ya Vuga mjini Zanzibar wakituhumiwa na mashitaka manne yanayohatarisha usalama wa taifa.
 
Waliofikishwa katika Mahakama hiyo ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu mjini Zanzibar Sheikhe Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe, Mselem Ali Mselem.
 
Wengine ni Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar.
 
Mbele ya Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Rayah Mselem alidai katika mahakama hiyo kuwa watuhumiwa wote kwa pamoja wanatuhumiwa kati ya Oktoba 17 na 18 mwaka huu mchana na mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, chini ya kifungu namba 16 kifungu kidogo cha tatu(d) sura ya 47 ya sheria ya Usalama wa Taifa, walitoa lugha ya uchochezi uliosababisha vurugu, ghasia na kuharibu mali yakiwemo majengo na barabara.
 
Mwendesha mashitaka huyo pia aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa, kati ya Mei 26, na Oktoba 19, mwaka huu, Viongozi hao waliwahamasisha wananchi mbalimbali wa mji wa zanzibar na viunga vyake kwa maneno ya uchochezi na kusababisha machafuko yaliyosababisha uhalibifu mkubwa wa mali katika maeneo mbalimbali ya mji wa zanzibar.
Rayah ameyataja maeneo ya mji wa Zanzibar yaliyoathiriwa zaidi na machafuko hayo kuwa ni Lumumba, Msumbiji, Fuoni, Meli Sita na Mbuyuni.
 
Hata hivyo watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kutokana na mashitaka yanayowakabili kuwa ni ya kuhatarisha usalama wa taifa.
 
Pamoja na watuhumiwa hao kudai na kuomba dhamana, mahakama hiyo haikuweza kutoa dhama kutokana na Hati ya iliyowasilishwa mahakamani hapo na Mkurugrnzi wa mashitaka wa zanzibar ya kuzuia dhamana za watuhumiwa hao chini ya kifungu namba 19 kifungu kidogo cha (1) na cha pili (2) sura ya 47 ya Sheria ya Usalama wa Taifa iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
 
Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande hadi Novemba 8, mwaka huu kesi yao itakapokuja tena kwa kutajwa.
 
Hiyo ni kesi ya pili kwa watuhumiwa saba na kesi ya kwanza kwa mtuhumiwa hao isipokuwa kwa mtuhumiwa wa nane Ghalib Ahmed Omari ambaye hiyo ni mara yake ya kwanza kufikishwa mahakamani.
 
Mtuhumiwa Galib ambaye alikuwa akitafutwa na Polisi kwa kuhusika na makosa yaliyompeleka mahakamani, alikamatwa juzi alipoonekana kwenye maeneo ya mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe kusikiliza kezi za wenzao.
 
Mara walipoondoka katika ukumbi wa Mahakama kuu ya Vuga, washitakiwa wote saba, walipelekwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe ambako nako jana pia walipaswa kwenda kusikiliza uwamuzi wa au watapatiwa dhama ama vinginevyo.
 
Hata hivyo mahakama hiyo kesi hiyo imetajwa tu na uwamuzi wa watuhumiwa kupewa au kutopewa dhama katika kesi hiyo ya kwanza utatolewa Novemba 7, mwaka huu.
 
Watuhumiwa hao wamerudishwa rumande katika Gereza la Chuo cha Mafunzo Ziwani.
   


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Mbona wamenyoa ndevu?

    ReplyDelete
  2. Mtakumbuka ushauri wangu mimi mwanasheria wa kujitegemea ughaibuni,kwamba sajilini hiyo jumuiya au chama chetu vyovyote mtakavyoita, halafu mnapo patashida namna hii sisi wanasheria tunawasimamia hatimaye kushinda,lakini mkanidharau na kunitukana,mnaona sasa, na nasema mtaishia pabaya.

    ReplyDelete
  3. sasa jamani hii mahakama kuu hata rangi jamani?

    ReplyDelete
  4. naamini hakuna refu lisilokuwa na mwisho. na mwisho wa aibu ni fedheha... inshalla Allah atawasaidia na kuwapa wepesi wa hali ya juu huko walipo masheikh wetu tuko pamoja nao....
    Jee huu si udhalilishaji kwa mahabusu hawa kuwanyoa ndevu???

    ReplyDelete


  5. Hawa viongozi wa uamsho me naomba wapewe nafasi wasema ukweli kuhusu kuharibu mali sababu hatuelewi kabisaa kila mmoja ana sema lake juu ya hili kundi

    ReplyDelete
  6. Hiyo mahakama kuu ni aibu tu.Hebu hao viongozi waache kwenda hizo trip za nje japo kwa miezi sita ili zipatikane fedha za kupakia rangi.

    ReplyDelete
  7. kwani huyu waziri wa sheria si hupatiwa fedha za matumizi kila mwaka, jee zina kwenda wapi? hawa viongozi maneno mda wao uishe tuwe na viongozi wanaojali maendeleo ya kweli. kama rangi bei mbaya basi hata chokaa twashindwa?

    ReplyDelete
  8. Yaani hata chokaa inashindwa kupakwa katika hiyo Mahakama tena Mahakama kuu. Posho ya safari ya siku mbili ya kiongozi mmoja inatosha kupaka rangi hata chokaa hilo jengo jamani, hii ni aibu halafi Zanzibar ni kamji kadogo na hizo ofisi za serikali ziko chache kinachoshindikana ni nini?

    ReplyDelete
  9. Serikali yetu tukufu haina dini. Inatawaliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi. Ukiingia huko gerezani hakuna shekhe wala padri. Ndevu utanyolewa utake usitake na kopo utanyea. Habari ndo hiyo. Andamaneni. Tutawanyoa. Ohoo!

    ReplyDelete
  10. ILITAKIWA WANYOLEWE NDEVU BAADA YA KUPATA HATIA YA KOSA LAO:

    Kwa nini Masheikh wanyolewe ndevu wakati Kesi bado inatajwa huku wakiwa bado ni WATUHUMIWA na hawajaingia ktk HATIA ?

    HILI NI KOSA LA KUMCHUKULIA MTUHUMIWA KAMA MFUNGWA KAMILI KWA KUMNYOA NDEVU!

    ReplyDelete
  11. Kama ni Utunzani wa Historia kwa nini angalau ukarabati bila kuvunja asilia usifanywe kwenye Jengo hili?

    Mbona Bagamoyo Wakandarasi wa Kampuniya Ujerumani wameweza kukarabati Majengo ya Kihistoria bila kuyabadili, iwe Zanzibar Mahakama Kuu?

    Hii ni Mahakama Kuu Zanzibar au Jumba Kuu la Makumbusho ya Historia Zanzibar?

    ReplyDelete
  12. wamenyolewa ndevu au wao wenyewe wameamua kunyowaa.

    eid mubaraka kwa viongozi wote wa uamsho hope wameruhusiwa kusali eid.


    mdau washington D.C

    ReplyDelete
  13. Kunyolewa ama Kunyoa ama vyote viwili nisheria za mahabusu/jela. Nywele ndevu za kidevuni ama bichwa ama popote pale mwilini ni hatarishi mtu aweza ficha humo vihatarishi kwa jela ama yeyemwenyewe ama wenziwake!! Tushuhulike na yaliyoyamsingi tuachane na midevu hiyo itaota tu mingine mcjali wadau!!
    Na hao mawakili wamechomoka kiakili... kaaazi mnayo!!

    ReplyDelete
  14. Duhh kumbe Sheikh Farid bonge la Brazameni!

    Cheki alivyokuwa handsome baada ya kunyolewa ndevu anapendeza, alikuwa anaonekana babu wa miaka 93 akiwa kijana wa miaka 39 kumbe midevu inazeesha wallahi.

    ReplyDelete
  15. Enhhh Sheikh Farid ana BABYFACE namna hii?

    Bora aingine ktk Siasa za CUF kama anavyoonyesha V ya Chadema isiwe kama sababu kuitumia UAMSHO kwa kuwa Dini abadani haikubaliani na vurugu!

    ReplyDelete
  16. Inategemea na msimamo wa mtu kuhusu ndevu:

    Isipokuwa vitu vitatu vimekuwa ni mtihani mkubwa kimaisha,

    1.Ndevu za kupindukia
    2.Mvi kichwani
    3.Upara (Uhalaza)

    Imeonekana watu wakihangaika sana kukwepa majaaliwa ya hivyo vitatu hapo juu, unakuta mtu anapata mvi ktk nywele anatumia super black kuzipaka nywele zake ziwe nyeusi, unakuta mtu ana kipara ananyoa unga kabisa kama fasheni huku akificha uhalaza au upara kichwani kwake.

    Unakuta mtu ana midevu anatumia wembe au kwenda saluni mara kwa mara hadi anaota vipele mashavuni kwa kukithirisha unyoaji.

    Ni jambo la ajabu sana kukuta mtu mwenye ndevu hazitaki ilhali unaweza kumkuta asie jaaliwa kuwa na ndevu yeye anazitaka!

    Nimeshawahi kumuona mtu hana upara/ uhalaza lakini anaenda saluni anaagiza anyolewe uhalaza!

    Unakuta mtu maejaaliwa na mvi hazitakai anaweka super black , hapo hapo unakuta asiye jaaliwa nazo anazitaka kwa kuweka rangi nyeupe kichwani!

    Basi ndio kama hivyo hayo majaaliwa tatatu juu yanatutiokea lakini watu wanatofautiana kuyakubali!

    ReplyDelete
  17. Ahhh Sheikh Farid Baza Kaka wa nguvu sema tu ni ule Msimamo Mkali wa Dini.

    Baada ya kunyoa ndevu bonge la Sharobarro!

    ReplyDelete
  18. Sheikh Farid unatuchanganya sasa je upo CUF au upo Chadema?

    Hiyo V ni alama ya Kilimanjaro bwa Shekhe !!!

    ReplyDelete
  19. Sheikh Farid kitu kibaya unachokifanya ni kuwaponza Maamuma wako nyuma kufikiri ya kuwa Harakati mazotekeleza ni za Dini kumbe ukweli mpo kwenye Siasa!

    Sasa si bora kama mlivyokwisha nyoa ndevu mkatoka kwenye U-Shekhe, kinachofuata mngevua Kanzu na Kofia za Vibaragashia vichwani kuvaa Kofia za Mapama, Kapelo na nguo za Vitenge vitenge na Magwanda ya Bluu ya CUF ???

    ReplyDelete
  20. Duhhh Serikali Ya Mapinduzi Zanzibar ngunguri si mchezo!

    Yaani na ubishi wote ule pale Zinjibar lakini Masheikh wenyewe wameelekea Kibla wamepunyuliwa ndevu zooooote wamepigwa wembe ndevu?

    ReplyDelete
  21. Nafikiri ni Bora mletwe Bara Magereza za ''Lupango'' ndio muelikike !!

    Pamoja na MAFUNZO YOTE HAYO huko ''CHUO CHA MAFUNZO'' BADO HAMJAELIMIKA NA KUJUA NINI UHALIFU WA MAKOSA YA JINAI KWA KUVUNJA SHERIA KWA VURUGU NA NINI NI HARAKATI ZA KISIASA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...