Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Lindi,Abdulaziz Ahmeid (Channel ten) akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji
wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa ,Reubern Mfune kufungua mafunzo ya
siku nne kwa wanahabari hao.
Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Bw Juma Thomas,Mwanasheria wa kujitegemea
akitoa mafunzo kwa wanahabari.
Wanahabari toka vyombo mbalimbali wakihudhuria mafunzo hayo
ili kujengewa uwezo wa kuandika kwa mujibu wa sheria Habari za
mahakamani.
Wanahabari wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Lindi wakiwa katika
Picha ya Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya
Ruangwa Bw Reubern Mfune mara baada ya kufungua mafunzo ya siku nne
kwa ya kuwajengea uwezo wanahabari...
kuhusiana na uandishi wa Habari za Mahakamani.
Wanahabari 18 wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Lindi kufuatia
mradi wa "Press club" Wameanza mafunzo ya uandishi wa habari za
mahakamani ikiwa ni mfululizo wa Mafunzo yanayoendeshwa na Umoja wa
Vilabu vya waandishi wa Tanzania.
Mafunzo hayo ya siku nne yanayoshirikisha wanahabari toka vyombo
mbalimbali yameanza jana Wilayani Ruangwa na kufunguliwa na Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri hiyo.
Baada ya mafunzo hayo Wanahabari hao watafanya mkutano mkuu wa mwaka
wa klabu hiyo ikifuatiwa na Mkutano wa Wadau wa Habari walio katika
wilaya hiyo
Mafunzo hayo yanayoendeshwa kwa ufadhili wa mradi wa Press Club Chini
ya Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzani(UTPC)Yameanza leo
wilayani Ruangwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...