Meya wa jiji la Arusha,Mstahiki Gaudence Lyimo (kushoto) akiwa katika maongezi na wasanii ambao walimfata kulalamikia kutoshirikishwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa jijini Arusha ikiwemo pamoja na kutopewa kipaumbele katika sikukuu za uzinduzi wa jiji la arusha (picha na woinde shizza,Arusha)
WASANII wa muziki na vikundi mbalimbali vya maigizo mkoani Arusha wamewataka viongozi wa serikali kutowadharau na kuwashirikisha kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo jijini Arusha.
hali hiyo imetokea wakati zikiwa zimebaki siku chache ili kufanyika uzinduzi rasmi wa Jiji la Arusha baada ya wasanii hao kudai kutoshirikisha kwa lolote.
akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake msanii wa muziki wa kizazi kipya Nakaaya Sumari alisema kuwa wameshangaa sana kusikia kuwa msanii kutoka dar es salaam Diamond Platnum atakuja kutumbuiza ilihali wao wapo na hawana taarifa yeyote.
nakaaya alisema kuwa hawana tatizo na Nasibu Abdul (Diamond) ila walichokiona ni dharau kutoka kwa afisa Utamaduni wa manispaa kwa kutoonyesha ushirikiano na badala yake wamepewa taarifa ya kufanya kitu jana usiku baada ya wao kuulizia.
"Tumeshanga sana hii ni dharau wasanii wa arusha hatuheshimiki kabisa na tumeuliza ndo tunaambiwa eti tuandae kitu kwa ajili ya uzinduzi dah yani inakatisha tamaa sana alafu afisa utamaduni mwenyewe anatuona anatupotezea"alisema nakaaya
Aidha nakaaya alimpongeza Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Gaudience Lyimo kwa kutoa ushirikiano wake kwao na kuahidi kushirikiana nao kwa madai ya kilichofanyika ni makosa ya kibinadamu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wasanii mkoa wa arusha Hussein Sechonge alikemea vikali tabia hiyo kwa kuwa wasanii wana mchango mkubwa wa kufikisha ujumbe na kuwataka viongozi kuwa wazalendo.
aidha walimtaka afisa utamadumi manispaa Juma Sule kutoa ushirikiano kwa wasanii wa hapa kwa kuwab wao ndio wanajua kila kitu kuhusu manispaa na sio Diamond..
''tunamshangaa sana hapa kuna wasanii 70 sasa nashangaa kwenye mwenge aliletwa Juma Nature wakati wao wapo hapa na hawafahaamu kitu chochote sio vizuri"alisema Sechonge
hadi mwandishi wa gazeti hili anaondoka katika ofisi za manispaa ya arusha wasanii hao walikuwa nje ya ofisi ya meya wakisubiri kujadiliana namna ya kufanya na kumaliza tofauti hiyo.
Excuse me ankal and wadau for the language am about to use, but I really have to say this: These AR artistes need to grow tha f up and act like real brands. If you aint got ish to do or say, you might as well lock yourself in and come up with ideas that will make you shine, products that will make you 'wantable'. Its not about regionalism or local-come-first basis, its about bringing results and your bankability. Events, be it government, corporate or even by NGOs need results when they are held, they need to push their agenda to the public, and so there is no sin in using brands and artistes that are associated with such - results, results and results, period! Why do you think major local music gigs (eg Fiesta) use award winning international millionaire artistes? Do you think the events hosts dont see local artistes in their radar? No, they see them but only as small bleeps, and so are always used as curtain raisers (unless one works hard to command a sold out show of 50,000 tsh plus per ticket and get to be ferried by a chopper to the venue). So always, international artiste will headline our gigs. The concept is the same for local events at regional level. Dar es salaam is synonymous to international, and regions are local. So when Diamond or Juma Nature is engaged to headline an event you local artistes need to stop whining and work hard so that next time you should be considered too. Its not about being from AR being an issue, its about what tha f are you doing to make fans, the media and the public want more of you. So when Diamond gets to headline a government/municipality event in Arusha, stop hating. Ask yourselves why is this guy the most bankable artist now? He must be doing something right (and his management too). So once again, no offense you guys (and anyone else who might take offense in this opinion), you need to grow tha f up. Act like real celebrities, stop hating and hustle hard!
ReplyDeleteOne love!
we nawe, kwahiyo ukiweka hiyo f ndio unajiona mmarekaniiiiiiiiii.
ReplyDeletewe nawe tuondokee we ndio wa kwanza unaetakiwa ku grow up maana hata hujui unaongelea nini usidahni kutumia lugha ya kigeni ndio kuongea ya maana na ma f.... ili iwe nini, waache waeleze concerns zao kama wameona wamedharaulia ni haki yao kuwasiliana na mamlaka husika waeleze kilio cha chao wao ndio wazawa wa arusha na wanaujua mji wao in out iweje leo aletww mtu kutoka mji mwingine agombee ubunge kwetu bwana?
ReplyDeleteMdau wa Canada una hoja,ila kwa mpira wa Bongo ni sawasawa na kumpigia Mbuzi gitaa.Huoni Yanga wanashindana na Simba kuleta makocha wa Kizungu na bado wanasumbuliwa na makocha wazawa,Kagera sugar,coastal union ni mifano halisi.Ni hayo tu
ReplyDeleteDavid V
Annon wa juu hapo unaoneka boya sana kwenye masuala ya uelewa. Wewe katika yote aliyosema jamaa wa kwanza we umeona hiyo F tu? Nyie ndo walewale waosha vinywa msokua na ushauri au maoni ya maana, siku zote ni kufungua midomo ili kutoa harufu mbaya tu, nothing else!
ReplyDelete