Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu na Mkurugenzi Mkuu wa TRA Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya.  wakimsikiliza Mkurungenzi Mtendaji anayeiwakilisha Afrika  Bw. Moeketsi Majoro  katika mkutano wa IMF nchini Japan- Tokyo

Mhe. Mgimwa na Mkurungenzi Mtedaji anayeiwakilisha Afrika IMF, Bw. Moeketsi Majoro  Naibu Katibu Mkuu Bw. S. Likwilile kwenye mkutano wa IMF  nchini Tokyo-Japan. Kushoto ni Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu na nyuma ni Bi. Mwanaidi Mtanda Mhasibu Mkuu wa Serikali.

Habari na pPicha na  Ingiahedi Mduma na
 Scola Malinga, Tokyo- Japan
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa kundi  namba moja la kanda  ya  Afrika anayewakilisha nchi za Afrika kwenye Shirika la Fedha la kimataifa (IMF) Bw. Moeketsi Majoro. Hivi karibuni Rais Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Dr. William Mgimwa kuwa Waziri wa Fedha nchini Tanzania ikiwa ni mara ya  kwanza akiwa kama Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki ya Dunia kuhudhuria Mikutano hii ya Benki ya Dunia na shirika la fedha la kimataifa inayofanyika hapa nchini Tokyo-Japan. 

Akiwa katika Mikutano hiyo, Mhe. Mgimwa amefanikiwa kuonana na Bw. Moeketsi na kufanya mazungumzo naye mbalimbali mojawapo likiwa ni jinsi gani Tanzania inaweza kufaidika na IMF na kuweza  kuinua uchumi wake kupitia shirika hilo. 

Akizungumza na Bw. Moeketsi, Mhe.Mgimwa alisema kuwa, ” Nina mambo muhimu kama manne ambayo ukisaidia kufikisha ujumbe huu na kama tutafanikiwa kupata fedha hizo tutakuwa tumepiga hatua sana katika kuinua uchumi wa nchi yetu. 

"Moja, ni kurekebisha barabara zetu na kuziweka  katika viwango vinavyotakiwa, pili ni mfumuko wa bei, kwakweli mfumuko wa bei umekuwa ukisababishwa na upandaji wa bei za bidhaa hasa vyakula  kama vile mahindi lakini tumegundua kuwa  mchele unapanda sana hata kuzidi mahindi, tatu ni hii hali ya Tanesco, kwa kweli umeme umekuwa ni tatizo kwetu pamoja na jitihada zote tunazozifanya na hasa za kutumia gesi.”alieleza Mgimwa. 

Aliendelea kusema kuwa  tunahitaji kuimarisha masoko ya ndani na kuwa na dhamana za kutosha, pamoja na kuwa tumeandaa mipango kamambe ambayo itatusaidia katika kutekeleza haya lakini bado tunahitaji nguvu kutoka shirika la fedha la kimataifa”.Naye  Bw. Moeketsi alifurahishwa na uelewa wa Mhe. Mgimwa na kumhaidi kufuatilia kwa karibu, kwani mambo yote aliyoyaeleza ni ya msingi na kwa sababu yako kwenye mpango mzuri yataweza kutekelezeka. Mazungumzo ya Mhe. Mgimwa na Bw. Moeketsi yamefungua mianya mipya na mahusiano ya karibu kati ya na shirika la  Fedha la kimataifa na nchi ya Tanzania.
 Mkutano huo ulihudhuriwa na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Bw. Benno Ndulu,Kamishna wa fedha za nje Bw. Said Magonya, Bi.Mwanaidi Mtanda ambaye ni Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw.Beda Shallanda ambaye ni Kamishna wa sera, Bi. Monica Mwamunyanye ambaye ni Kamishna wa Bajeti, Bw. Ahmed Rutashobola ambaye ni mwakilishi wa Tanzania huko IMF na baadhi ya maafisa kutoka Benki kuu na Wizara ya fedha . Aidha Mhe. Mgimwa alimalizia kwa kueleza kuwa Tanzania imejitahidi sana kupunguza deni la Taifa na vilevile inafanya jitihada za kuimarisha usimamiaji wa deni hilo kwa kuhamishia jukumu hilo Wizara ya Fedha ili kuweka usimamizi na udhibiti wa karibu zaidi.
Nchi za Afrika zimegawanywa katika makundi matatu na Bw. Moeketsi anaziwakilisha nchi ishirini na moja za Afrika ambazo ziko kwenye kundi la kwanza.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...