Waziri wa fedha Dk. William Mgimwa akiongea wakati wa uzinduzi wa kutumia huduma ya Faraja Bima kupitia M-pesa kwa kushirikiana na Heritage Insurance,uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa huduma ya Faraja Bima itakayopatika kupitia M-pesa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Heritage Insurance Bw.Paul Lewis akisema machache wakati wa uzinduzi huo.
Ofisa Mkuu wa M-Biashara wa Vodacom Jacques Voogtz (Katikati) akimuonyesha Waziri wa fedha Dk. William Mgimwa namna ya kujiunga na kutumia huduma ya Faraja Bima kupitia M-pesa baada ya kuizindua jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza. Kupitia Faraja bima mteja anweza kulipia bima yake kwa M-pesa.
Waziri wa fedha Dk.William Mgimwa akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza na Mkurugenzi Mtendaji wa Heritage Insurance Bw.Paul Lewis.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingwa kushoto akimsikiliza jambo Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu, watatu toka kushoto wakati wa uzinduzi wa kutumia huduma ya Faraja Bima kupitia M-pesa,wapili kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania Bw.Salum Mwalim na kulia ni Angela Sompet.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. dada rukia nakumbuka enzi zile nikiwa tz nilikuwa napenda kukuangalia ukitangaza taarifa ya habari itv...naona siku zimekwenda kwelikweli umekuwa mama sasa..hongera..mdau sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...