Baadhi
ya Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa wanasubiri treni ya mwakyembe iwasili
stesheni ikitokea ubungo maziwa tayari kwa safari ya kuwarudisha
Majumbani Kwao. Baadhi ya Abiria wakiwa wamewahi kwaajili ya Kupanga
foleni ili waweze kupata siti huku wengine wakichuchumaa kutokana na
kulisubiri kwa muda
Abiria
Wakiteremka katika treni linalofanya safari zake ndani ya Jiji la Dar
mara lilipowasili Katika Kituo cha Stesheni karibu na central polisi
tayari kwa safari ya kurudi tena Ubungo
Baadhi
ya Abiria waliogeuza na treni hilo wakiwa wamepandia Kituo cha Kamata
Ili kuwahi Siti ambapo walipelekea sintofahamu kwa baadhi ya abiria
waliokuwa kituoni hapo na kutaka kupanda kwenye hilo behewa kukuta
likiwa tayari limeshajaa kutoka na abiria kugeuza na treni hilo wakati
utaratibu huwa haurusiwi na ikifika mwisho abiria wote wanatakiwa
kushuka
Abiria
wakianza kupanda treni tayari kwa kurejea makwao mara baada ya treni la
mwakyembe kuwasili kituoni hapo kwenye majira ya saa kumi na moja na
dakika ishirini jana
Mmoja
wa Abiria aliyegeuza na treni hilo ambapo walipandia Kamata kwa lengo
la kuwahi kiti akibishana na mmoja katika ya abiria ambao walikua kwenye
foleni muda mrefu wakisubiria treni hilo kufika ili waweze kuingia
ndani na kupata siti ambapo alikuta behewa hilo likiwa limeshajaa na
kuanza kubishana huku abiria waliokuwa wakisubiri treni hilo wakitaka
abiria waliogeuza na treni hilo kushuka
Wakazi
wa Jiji la Dar wakiwa kwenye foleni ya kupanda treni maarufu kwa jina
la treni ya mwakyembe jana kwenye majira ya saa 11 jioni katika kituo
cha Stesheni tayari kwa kurudi nalo ubungo huku baadhi ya behewa kuwa
limeshajaa kabla hata halijafika kituoni hapo kutokana na abiria kugeuza
nalo kwa lengo la kuwahi siti. Behewa ambalo lilikuja likiwa limeshajaa
ni behewa lenye namba 3644 ambalo abiria wake walikua wamepandia njiani
kwa nia ya kugeuza nalo ili waweze kupata siti.
Wakazi
wa jiji la Dar wakipanda kwenye treni la mwakyembe mara baada ya
kuwasili kwenye kituo chake cha Stesheni jana Kwenye majira ya Saa 11
Jioni jana tayari kwa kuwarudisha majumbani kwao likitokea Mjini
kuelekea Ubungo ambapo ndio kituo cha Mwisho
Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
Katika
hali isiyo ya kawaida jana kwenye majira ya Saa 11: 20 Jioni katika
kituo cha Treni kilichopo stesheni mkabala na Kituo Cha Polisi Cha
Cetral kuliibuka Jambo la kushangaza wakati abiria wanaosubiria treni
inayofanya kazi zake ndani ya jiji la dar kuona behewa moja likiwa
limeshajaa tayari kutokana na abiria kupandia njiani na kugeuza nalo
kwa lengo la kuwahi siti na kupelekea abiria waliowahi kituoni hapo na
kupanga foleni kwaajili ya kuwahi siti kuambulia patupu.
Abiria
waliokuwa wakisubiria treni hilo walianza kulalamika pale ambapo
walikuta behewa hilo limeshajaa kabla hata treni hiyo haijafika kwenye
kituo chake cha mwisho kwa lengo la abiria hao kuwahi .
Baada ya Tukio hilo kutokea kulizuka sintofahamu kwa baadhi ya wafanyakazi na Askari Polisi ambao hawajawahi kuona utaratibu huo ukifanyika na kupelekea Abiria kuhisi tayari wafanyakazi wa treni hiyo waneshaanza kuchakua kitu ambacho utaratibu hauruhusu.
Utaratibu uliopo ni kwamba hata kama abiria amepandia katikati anatakiwa kuteremka pindi treni hilo linapofika mwisho wa kituo ndipo akate tiketi kwaajili ya kupanda tena na kurudi nalo lakini hali imekuwa tofauti hapo jana baada ya abiria hao kutokushuka na tiketi kukatiwa ndani na kupelekea abiria waliokuwa wakisubiri treni hilo kusubiri kwa muda mrefu.
Baada ya Tukio hilo kutokea kulizuka sintofahamu kwa baadhi ya wafanyakazi na Askari Polisi ambao hawajawahi kuona utaratibu huo ukifanyika na kupelekea Abiria kuhisi tayari wafanyakazi wa treni hiyo waneshaanza kuchakua kitu ambacho utaratibu hauruhusu.
Utaratibu uliopo ni kwamba hata kama abiria amepandia katikati anatakiwa kuteremka pindi treni hilo linapofika mwisho wa kituo ndipo akate tiketi kwaajili ya kupanda tena na kurudi nalo lakini hali imekuwa tofauti hapo jana baada ya abiria hao kutokushuka na tiketi kukatiwa ndani na kupelekea abiria waliokuwa wakisubiri treni hilo kusubiri kwa muda mrefu.
Lukaza
blog imeweza kunakili sauti za abiria ambao waliokuwa wakilalamika juu
ya utaratibu huo uliofanywa na wafanyakazi ambao sio waaminifu na
kupelekea usumbufu kwa abiria ambao wamewahi kupanga foleni.


aibu kubwa sana kweli bongo bado tupo nyumba miaka 100, hivi kweli tokea lini train likatumia mlango mmoja tu kwajili ya kupandia abiria na kushukia?
ReplyDeletena hivi inashindikana vipi kuweka ukuta au kijukwaa cha kushukia train au kupandia ? watu wanashuka na kupanda ngazi za train ni hatari sana wanaweza kusababisha kuvunja kwa miguu
hivi watu wazima wanawezaje kupanda hilo train?
mnatuaibisha sana serikali baada ya kututoa kimaso mnatupakazia kuwa na train za ajabu kama hizo huduma mbovu foleni utasema sukari enzi za nyerere
aibu aibu aibu kubwa.
Usafiri wa Mjini kwa Treni,
ReplyDeleteNi usafiri wa Halaiki, hivyo msitegemee kuwa lazima abiria upate kiti!
Huu ni usafiri wa kuwa tayari kwa kusimama ikibidi, acheni mipango yenu mibovu ya kwenye Mabasi ya kugeuza nalo kama mnavyo fanya asubuhi: MkIwepo,
-Ukonga Banana na Ukonga Mombasa kugeuza nalo Gongolamboto kurudi na basi Posta.
-Kimara Baruti na Kimara Bonyokwa, kwenda Kimara mwisho na Kurudi na basi Posta
-Mbagala Zakhem kugeuza na basi Mbagala Rangi 3 na kurudi na basi Posta.
Mjaribu kubadilika na kuukubali mpango mpya wa usafiri kwa manufaa ya wengi!!!
Huo ni ubwege mtozeni kwa nini mgeuze na mabasi kama Mataahira?
ReplyDeleteHuo ni ubwege mtozeni kwa nini mgeuze na mabasi kama Mataahira?
ReplyDeleteKama mmesha anza kugeuza na Treni ya MWAKYEMBE ni moja kwa moja, hata katika Mpango wa Mabasi yaendayo kasi ya MAGUFULI mtakuwa mnageuza nayo!!!
ReplyDeleteWatanzania tustaarabike.hii itasaidia kuwapa moyo viongozi wetu kuendelea kuleta maendeleo.TUBADILIKE!!
ReplyDeleteAngalieni Wabongo hawa!
ReplyDeleteSasa wajameni hizi Treni ni za safari za Mjini mnageuza nayo wakati safari yenyewe inachukua sio zaidi ya saa 1 au chini ya Dakika 60, kwani mkae kwenye viti mnakwenda Tabora au Kigoma?
Nadhani kwa kuwa nia ya watoa huduma ni kutoa huduma iliyo bora nadhani kwa upande mwingine nauli ya mtu anayegeuza na gari moshi iwe mara tatu ili kuchuja mzunguko huo. ER
ReplyDeleteDa kazi kweli kweli, halafu unaambiwa Bongo tambarale.
ReplyDelete