Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) unaheshima kubwa kutarifu na kuwaomba watanzania wote wanaoishi ujerumani na jirani ya Ujerumani kuwa umoja wetu tunatarajia kufanya hafla ya kumuaga Mheshimiwa balozi Ahmada Ngemera (katikati) ambaye anamaliza muda wake wa kufanya kazi, hafla hiyo itafanyika mjini Berlin siku ya Jumamosi tarehe 8.12.2012 .

Mhe.Balozi Ahmada Ngemera amekua balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na watanzania wanaoishi ujerumani watamkumbuka daima Mheshimiwa Balozi kwa kuwa karibu sana na jamii ya watanzania,pia atakumbukwa kwa jitihada zake au kile ambacho watanzania wa ujerumani wanachokiita kuasisi Umoja na mshikamano wa watanzania nchi ujerumani,ambapo Mhe.Balozi Ngemera na msaidizi wake Mhe. Ali Siwa waliutumua kuhamasisha watanzania waishio Ujerumani kuungana katika kila hali kuanzisha umoja wa mshikamano wa watanzania,kitu ambacho mabalozi wengi walishindwa kufanikiwa kufanya labda kwa sababu ya ukubwa wa nchi ya ujerumani wa watanzania wanaishi katika miji mbali mbali.

Lakini kazi hiyo ya kuwaunganisha watanzania, Balozi Ahmada Ngemera na Msaidizi wake Bw. Ali Siwa walifanikiwa kuwafikia watanzania wote waishio Ujerumani na kuwashauri waanzishe umoja wa mshikimano,na matunda ya juhudi zao ndipo kukazaliwa Umoja wa waTanzania Ujerumani.(UTU) Umoja ambao ni chombo cha watanzania wote ! chombo ambacho watanzania waishio ujerumani wanajivunia ! UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO MSINGI WETU IMARA!

OMBI:

TUNAWAOMBA WATANZANIA WOTE ! NA MARAFIKI WOTE WA TANZANIA AMBAO WANATAKA KUSHIRIKI KATIKA HAFLA HII, TUNAOMBA MTOE MCHANGO WA EURO 20.00 NA KWA WANAFUNZI EURO 10.00 TU

kwa kupitia Account : Union of Tanzania in German e.V.

VR Bank Rosenheim-Chiemsee AG Konto-No.: 59641 BLZ: 71160161 Verwendungszweck: „Kumuaga Mhe. Balozi Ngemera

Pia unaweza kuwasiliana na kamati.utu@googlemail.com simu namba +491734297997 au Katibu simu namba 01734744265 .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nimesikitika sana kusikia kuwa mh balozi
    anamaliza muda wake hapa Ujerumani, kwa kweli tutammiss sana, amekuwa akituunganisha kwa mambo mengi. Sasa swali je, hizo Euro 20.00 sina shaka kuzilipa, mbona hamjasema sherehe ya kumuaga itakuwa kwenye ukumbi gani?
    Au tunatoa tu na ndiyo mwisho wa mambo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...