BENDI Kongwe ya mziki wa dansi nchini Tanzania Msondo Music inatarajia kuzindua vyombo vyake vipya kabisa walivyokabidhiwa hivi karibuni na Kampuni ya KONYAGI.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema wameshapewa vyombo hivyo na Konyagi ambavyo vitazinduliwa mbele ya mashabiki lukuki wa bendi hiyo siku ya Ijumaa pale LIDAZ CLUB hivyo wapenzi wote wa bendi ya Msondo mnaombwa kuhudhuria kwa wingi ili kuona vyombo vipya Pamoja na kupata burudani za bendi hiyo zikiwemo nyimbo za zamani na za sasa kwa ajili ya kuanza wik end.

 Super D aliongeza kwa kusema wapenzi watakaokuja siku hiyo watapata burudani za radha tofauti tofauti kwani wamepanga kukonga nyoyo za mashabiki wao kwa kutumia vyombo vyao vipya.

Bendi hiyo siku ya Jumapili itamaliza burudani za wik end katika ukumbi wa Max Bar Ilala bungoni.

    Mkurugenzi wa Bendi hiyo Muhidini Maalimu Gulumo ataongoza kundi zima la wana msondo ngoma akiwemo Said Mabera,Shabani Dede, Romani Mn'gande, Eddo Sanga, Juma Katundu, Hassani Moshi na wendine kibao kwa ajili ya kuwaburudisha mashabiki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...