Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere akiwa kwenye gari aina ya Land Rover 109 ya Halmashauri ya Wilaya ya Mafia wakati alipotembelea Wilaya hiyo wakati  akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. MWALIMU HAKUWA NA MAKUU,HAKUPENDA KUTUKUZWA,NA KUNA WAKATI ALISHAURI HATAKI MSURURU MREFU WA MAGARI AWAPO KWENYE ZIARA ZA KIKAZI,ALIKUWA MKALI SANA KWENYE MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA.LEO HII IKOJE WADAU?MAGARI YA KIFAHARI VX V8,X5,LAKINI WAGONJWA WABEBWE KWENYE BAJAJ.WATAWALA WETU NAONA HATA BARABARA WANGEPENDA WAJENGEWE ZA KWAO TU.

    ReplyDelete
  2. Huyu ndio alikuwa raisi. Alipanda landrover 109 hakutaka magari ya kifahari kama leo tuwaonavyo viongozi wetu, yote hayo ili mtoto wa maskini asome bure elimu ya uhakika sio ya kijanjanja ya leo, maskini atibiwe bure.

    Tutakukumbuka daima, pamoja na watu wanachafua taswira yako lakini bado upo mioyoni mwa Watanzania Wakristo kwa Waislam.

    Nyerere atabaki kuwa peke yake mpaka sasa, Baba wa Taifa Julius Nyerere

    ReplyDelete
  3. MWALIMU ALIKUWA MTU WA WATU ,HAKUPENDA MAKUU.TOFAUTI SANA NA VIONGOZI WETU WA SASA.ALIPENDA KUWA SAWA NA WENGINE,KAMA MTU WA KAWAIDA SANA.UKALI WAKE ULISAIDIA SANA WALIO CHINI YAKE WAOGOPE KUJILIMBIKIZIA MALI.LEO HII MAMBO NI TOFAUTI KABISA.ANGALIA TANESCO LIMEKUWA SHAMBA LA BIBI,MTU KAMPA TENDA MKEWE,KWELI?NA YUPO ANATANUA.

    ReplyDelete
  4. Nchi wakati huo ilikuwa ya NIDHAMU sana kuanzia utunzaji wa magari na vifaa vya UMMA.
    Mwalimu alitupa mwongozo mzuri sana BALI waliokuja WALIHARIBU Nchi kabisa.

    ReplyDelete
  5. Enzi hizo lazima upige kishoka athi!

    ReplyDelete
  6. Duh ilikuwa mwaka gani hii?.Hapa sasa ndipo utajua umuhimu wa Picha.Ankal utakuwa nazo nyingi za aina hii mkuu.Kwanini usiwe unatuwekea bwana,mambo ya down Memory Lane(Kila Jumamosi)nakumbuka mwaka 1977 Malimu(pumzika kwa amani) alikuja Wilayani kwetu nikiwa mdogo na msafara wa hizi 109.

    WAKAZI WA UK:Hizi Landlover 109 bado zipo?zinapatikana sokoni nikihitaji used,say pick up naweza kuipata?

    David V

    ReplyDelete
  7. Zama ni ni mwendo wa Toyota Land Cruiser V8.

    ReplyDelete
  8. Gari hizo ndizo zilikua kali na zinazoweza kupita popote, Vx,v8 hazikuwepo kipindi hicho na zingekuwepo angetumia tu msijidanganye,..kumbukeni wakati huo kila kitu kilikua adimu mpaka hata sabuni ya kuogea, ni vizuri kuona tulikotoka ni mbali na shida nyingi ,lakini kumsifia tuu mtu bila vigezo vya kweli sote tutakua ni watu tusiotafakari vyema.

    ReplyDelete
  9. Hivi mnapajua Mafia ninyi? Hakuwa na chaguo mbona hamjiulizi ilikuwaje Raisi apande gari la mkuu wa wilaya? hadi leo hii Mafia hakuna magari ya maana na ndio maana viongozi wa kitaifa hawaendi huko.

    ReplyDelete
  10. Kweli kabisa anon wa 08:32:00 AM.

    Ingekuwa leo angepanda VX. Mbona akiwa Dar alikuwa anapanda MERCEDES BENZ na siyo 109? si angepanda pijo 504? au corolla? au hilohilo 109? si hana makuu?

    Alituambia friji na TV ni LUXURY wakati yeye alikuwa na TV ili aangalie yeye tu halafu anatuambia kaota kumbe kaona kwenye TV.
    Tusimsifie kinafiki, kama hakupenda makuu mbona alikuwa na ndege zake peke yake? si angekataa na kukifunga kitengo? na angekodi? kuna kubwa kama kuwa na ndege yako mwenyewe?
    Mbona hakupanda corolla? si angekataa mabenzi?

    Kupanda VX au X5 siyo makuu, ni status.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...