Michoro ya sehemu mradi mkubwa wa bomba la gesi asilia linalotoka Mtwara hadi eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam uliozinduliwa na Rais Kikwete hivi majuzi.

Mradi huo, unaojengwa China National Petroleum Corporation (CNPC) unatarajiwa kumaliza kabisa tatizo la umeme wa mgawo ifikapo mwaka 2015 kwa kuzalisha megawati 3,000 ambazo ni zaidi ya mahitaji ya umeme kwa sasa. 

Kwa kuanzia mradi utaanza kwa kuzalisha megawati 900 na ifikapo 2015 utakuwa unazalisha megawati 3,000 na kufanya mgawo wa umeme kuwa historia. Tafiti za kitaalamu zinaonyesha kuwa kiwango cha gesi kilichopo eneo la nchi kavu Tanzania kinaweza kutumika kwa miaka 90 kwa matumizi ya hapa nchini na kuuza nje ya nchi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. ILANI.
    Jamani gesi ndio hiyo inaletwa na hatimae itasambazwa kila mahali kwa matumizi ya nyumbani; wasiwasi wangu ni kwamba kama hatutakuwa waangalifu katika namna ya kuishughulikia matokeo yake tutakuja kuunguzana ndevu. Madhara ya gesi ni makubwa mno kuliko hata madhara ya umeme, kwa hiyo patahitajika nidhamu na tahadhari ya hali ya juu ili kuchunga usalama.
    Ninachoomba ni kwamba wizara husika ifanye juhudi za haraka katika kutayarisha sheria kali za tahadhari katika maeneo mbali mbali na hasa ingefaa zitumike sheria za kimataifa.
    :Kwa mfano katika kusafirisha, chupa za gesi ziwekwe vipi, na magari aina gani kuruhusiwa kubeba.
    :Mafunzo ya nguvu, kwenye vyuo vya ufundi kwa mafundi watakaohusika.
    :Waruhusiwe mafundi wenye leseni tu ambao watakuwa wamefuzu mafunzo.

    ReplyDelete
  2. Asante kwa taarifa.Mradi muhimu sana kwa uchumi wa nchi.Swali dogo la nyongeza..kwa kuwa wananchi wanaofaidika na kupata tabu ya mgao wa umeme wengi wako mijini(~90%),na kwa kuwa vijiji vingi nchini Tanzania havina umeme(hata huo wa mgao)..Je hizo megawati 3000 zinazozungumziwa hapa zinajumuisha pia wananchi wanaoishi vijijini?na ni lini vijiji vyote vya Tanzania vitafaidika na mradi huu?

    David V

    ReplyDelete
  3. ni kweli mdau wa pili.

    ReplyDelete
  4. Mimi nadhani wadau hamjasoma vizuri maelezo. Hii siyo gas ya kupikia. Ni gas itakayotumika kuzalisha umeme. Sidhani kama hapa wanaongelea gas ya matumizi ya nyumbani. Watatumia natural gas kuzalisha umeme kwahiyo bado hilo suala la kuunguza nyumba halipo hapa. Japokuwa tutakapoanza usambazaji wa gas majumbani ndo moto utawaka. Nasisi tulivyo wazembe...kama watu wata-treat gas kama maji kweli watanzania wengi watapoteza maisha na kuwa vilema wa kudumu. Mungu ibariki Tanzania. Mdau, CA-USA

    ReplyDelete
  5. umeme utatokana na rasilimali zetu,hawa tanesco waache tabia mara moja kutuuzia umeme wa bei mbaya kiasi ambacho mwananch wa chini hawezi kuulipia bills.

    Matumizi ya gas kwa majumbani wizara husika iyandae mpangop maalum kama insurance kwa yoyote atakae pata madhara na kulipwa fidia,bila ya hivyo tunaweza tukateketea kwa rasilimali zetu wenyewe na wakubwa kunufaika na rasilimali hizi.

    Elimu itahitajika kwa watumiaji wa gas majumbani,kuwe na watu maalum wa ku install gas katika majumba,na watu wawe wamepatiwa vibali maalum kutoka kwa wizara husika ,sio kutuvurundia majumbani mwetu na kutkomea na kutusababishia ajali majumbani

    Tatu imagencey inahitajika na iyongwezwe kwa vungu zaidi,kila eneo kuwe na imagince fire,wakati wowote wakihitajika wafika kwa haraka,itasaidia kupambana na ajali mara kwa mara kutotuathiri zaidi.

    Nawakilisha mdau Munda.

    ReplyDelete
  6. Pamoja na uzuri wa mradi huu, kupatikana kwa umeme bila kuimarisha miundo mbinu hasa ma transfoma yanalipuka kila kisu, mgao wa umeme kuisha itakuwa ndoto!

    ReplyDelete
  7. Mdau CA-USA.
    Gesi inayotumika kuendeesha turbine za umeme na ile ya kupikia tofauti yake ni namna ya kui-process tu. Mradi bomba la natura-gas likishafika Kinyerezi kinachohitajika ni mitambo ya kui-process, na sio kama kutajengwa bomba jingine. Kwa hiyo kwa vyovyote vile bomba hili hili ndilo hatimae litatufanya tupate hiyo gesi ya majumbani baada ya mda si mrefu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...