Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Geofrey Meena Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kuitambua kwa mchango wake katika mapambano dhidi ya Malaria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupambana na ugonjwa huo inayoitwa (Malaria Safe Companys) uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam jijini dar es salaam jana.ambapo Wizara ya afya inashirikiana pamoja na taasisi za kimataifa na Makampuni mbalimbali pamoja na Sekta ya michezo, ambapo wadau mbalimbali wameshiriki katika uzinduzi huo.
 
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Mh. Hussein Mwinyi akimpongeza Bw. Geofrey Meena baada ya kupokea cheti hicho kwa niaba ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Mzee CHrisant Mzindakaya Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuzalisha nyama ya mkoani Rukwa kwa mchango wake katika kupambana na Malaria nchini.
 
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wadau makampuni na taasisi mbalimbali wanaopambana na ugonjwa wa malaria nchini mara baada ya uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...