Serikali ya Tanzania imekitaka kituo cha televisheni cha Kimataifa cha CNN kusahihisha taarifa potofu ilizotoa kuhusu mgogoro wa mpaka unaoendelea kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa.

Taarifa hizo zinaonyesha kwamba mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa upo kwenye ufukwe wa Pwani ya Tanzania jambo ambalo Serikali imesema siyo sahihi.

Akiongea na waaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Assah Mwambene amesema Serikali ya Tanzania imesikitishwa sana na taarifa hiyo na kuitaka CNN kuisahihisha mara moja.

“Tumesikitishwa sana na taarifa hiyo na tunashangaa kuona chombo kikubwa kama CNN wanaweza kutoa taarifa za uongo kwa kiasi hicho” amesema Bw. Mwambene.

Amesema ukweli ni kwamba unapozungumia eneo la Tanzania kilometa za mraba 947,300 (947,300 sq km)  ikiwa ni pamoja na  nusu ya eneo la ziwa kaskazini mwa mpaka wa Tanzania na Msumbiji na kwamba mpaka upo katikati ya ziwa kama ilivyo kwa mpaka wa Malawi na Msumbiji.

Kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 24 Novemba, 2012, CNN International yenye makao yake Makuu nchini Marekani  imekuwa ikiendesha  kipindi kuhusu mgogoro wa Tanzania na Malawi na kuonyesha kwamba mpaka uko pembezoni mwa ufukwe wa Tanzania.

Bw. Mwambene amesema kuwa suala hilo hivi sasa linatarajiwa kupelekwa katika Baraza la Marais wastaafu wa Nchi za Umoja wa SADC kwa ajili ya kulitafutia ufumbuzi.

Wakati huo huo, Sherehe za miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania bara zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9 mwaka huu.

Kauli mbiu za sherehe za uhuru mwaka huu ni uwajibikaji , uadilifu na uzalendo ni nguzo ya maendeleo ya Taifa letu.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. nisaidieni jamani, uhuru wa Tanzania bara au Uhuru wa Tanganyika?

    ReplyDelete
  2. Moja kwa moja Mchawi wetu ktk suala hili la Ziwa ni Marekani!

    Mnaona sasa?

    Hawa jamaa Wamarekani wana kawaida ya kutumia sana vyombo vyao vya habari ili kufikia malengo, hapo ina maana ya kuwa kwenye mapatanishano ni lazima Mpatanishi atalazimishwa kuchukua msimamo huo wa Marekani kuwa Mpaka upo ufukweni!

    ReplyDelete
  3. Malawi wamehangaika na wamefika CNN wanaitumia ili kufikia malengo yao.

    ReplyDelete
  4. Hao hao CNN wanatakiwa walazimishwe na Tanzania kuendesha Kipindi kingine ili kusahihisha upotofu wao.

    1.Kwa kuwa suala bado lipo ktk Kikao hawakuwa na uhalali wa kutoa taarifa hizo potofu.

    2.Ni lazima waendeshe Kipindi ili kusahihisha uongo wao.

    3.Wao sio Mahakama wala chombo cha Mamlaka ya Kimataida kama UN , Un yenyewe haijasimama kutoa taarifa yeyote kwa nini wao CNN wakurupuke?

    NI LAZIMA WARUSHE KIPINDI KUIOMBA MSAMAHA TANZANIA DUNIA NZIMA

    ReplyDelete
  5. HADHI YA CNN IMESHUKA KIASI KIKUBWA BINAFSI SISHANGAZWI NA TAARIFA HIYO KWA SABABU ZAMANI NILIKUWA MPENZI MKUBWA WA KITUO HICHO KWA KUPATA HABARI,LAKINI BAADA YA MIAKA KARIBU KUMI NIKAAMUA KUKIHAMA KWA KUWA WANA TABIA YA KUELEMEA UPANDE MMOJA KATIKA KUTOA HABARI ZAO KITU AMBACHO NI CHA KAWAIDA VYA VITUO VYA HABARI VYA HAPA AMERIKA KAMA FOX NEWS NA MSNBC.
    SASA CNN HAWAJAJITOA WAZI LAKINI TAARIFA ZAO ZA MATUKIO YA ULIMWENGUNI SIKU ZOTE HUEGEMEA UPANDE WANAOTAKA WAO INABIDI UWE MCHAMBUZI WA KUCHUJA HABARI VEMA ILI UGUNDUE HILO KWA HIYO KUHUSU MGOGORO HUU WA ZIWA NYASA WAO WAMEHAMIA MALAWI KWA KUWA KISIASA MALAWI WAKO KARIBU SANA NA MAREKANI NA TANZANIA WANATUONA KAMA URUSI.
    HABARI ZA UHAKIKA UKITAKA BORA USIKILIZE NA KUANGALIA AL-JAZEERA IN ENGLISH UNAWEZA UKAPATA HABARI SAHIHI AMBAZO HAZINA UPENDELEO.
    MDAU.
    COLORADO.

    ReplyDelete
  6. Mhe.Assah Mwambene,

    Ahsante kwa Taarifa hii, mahala pa kuanzia ni hapo hapo CNN na sisi Tanzania tupeleke makala yetu ili kurekebisha Taarifa za upotoshaji zilizorushwa duniani waandae kipindi cha Tanzania kama wao Malawi walivyowafanyia,

    CNN kama wao hawana muda na nchi masikini kama Malawi kurusha taarifa zao kama wao Malawi hawakuwa wamepeleka Makala Kipindi kiandaliwe.

    DUNIA NI LAZIMA IFUNDISHWE YA KUWA

    1.KAMA HUWEZI KUWATUMIKIA MABWANA WAWILI KWA WAKATI MMOJA, VIVYO HIVYO HUWEZI KUTUMIKIA SHERIA MBILI MOJA YA MKOLONI(Mkataba wa Heligoland wa 1890) NA INGINE MPYA(Sheria mpya za Kimataifa za mipaka ya kwenye maji baada ya UN kuasisiwa mwaka 1945) KWA WAKATI MMOJA.

    2.DUNIA LAZIMA IKUMBUSHWE YA KUWA KTK SHERIA SHERIA MPYA INAUWA SHERIA NA MIKATABA YA ZAMANI, HIVYO MAKUBALINAO HAYO YA HELIGOLAND YA MWAKA 1890 YAMEZIKWA NA SHERIA MPYA ZA MIPAKA ZA UMOJA WA MATAIFA ZILIAOANZA KUTUMIKA KUANZIA MWAKA 1945.

    3.HIVYO DUNIA HAIWEZI KUTEKELEZA SHERIA ZA MKOLONI NA KUZINGATIA MIKATABA YA MKOLONI YA MWAKA 1890 WAKATI HUO HUO IKIZINGATIA NA KUFUATA SHERIA MPYA ZA MIPAKA YA KIMATAIFA.

    ReplyDelete
  7. Nyerere alipoweka Mpaka kwenye maji aliona mbali kwa kuwa Wakoloni kuuweka Mpaka ukingoni ktk Mkataba wao wa Heligoland wa mwaka 1890 walikuwa wamechemka kinyume na Sheria za Kimataifa za mipaka ya kwenye maji (mipaka hupita katikati ya maji).

    Hivyo Nyerere alikuwa sahihi kuliko Mkoloni!!!

    ReplyDelete
  8. Sasa jamani CNN ni station ya kimataifa na ninyi mnalalamika bila kununua airtime kwenye mtandao wao ili mjitetee...!! Nunueni airtime hata dakika 5 mkafafanue hili suala. Nunueni airtime BBC, Al Jazeera na CNN ili mukanushe. Kulalamika na kuwaonya kwa barua hakutasaidia au kubadili chochote. Waziri wa mambo ya nje na wa sijui ni ardhi na wahusika wengine waende wakahojiwe CNN wajitetee...!!
    Mdau, CA-USA

    ReplyDelete
  9. CNN ni mdomo wa Watawala wa dunia.. Hivyo wakisemacho hakuna wa kukipinga

    ReplyDelete
  10. Waache waseme watakavyo,mnahangaika nao wa nini hao CNN,na siyo mpaka tu wanatusema vibaya kila Idara hao washenzi wa CNN.Sisi(Watz) tunachofahamu ni kwamba mpaka unapita katikati ya ziwa.FULL STOP.Hakuna kulegeza kamba vijana tupo tayari."Tumevumilia sana...tumenyanyaswa sana...Unyonge wetu...."(Mwl.J.K Nyerere)

    David V

    ReplyDelete
  11. Uwajibikaji sawa tutawajibika ila hawa wasio waadilifu na waliokosa uzalendo na kuamua kuiba fedha na kuficha mbali au hawa wanaosaini mikataba kwa ufisadi lazima tuwafanye kitu mbaya ili turudishe imani kwa wananchi vinginevyo uwajibikaji,uadilifu na uzalendo vitaishia ktk levo ya kauli mbiu tu.

    ReplyDelete
  12. Mimi nafikiri Cnn wanatumiwa tu, lakini nafikiri kuna njama za kutaka ku-destabilise nchi zetu hizi kwa faida ya wakubwa, kama wanavyofanikiwa kwenye nchi za kiarabu.
    Mradi wameshaanza kusema hivyo basi ujue kuna mengine mengi yapo njiani. Na tusije kuona ajabu tukija kuona nchi kubwa kati ya hizi zinazojifanya eti ni marafiki zetu kuja kutugeuka.
    Wao kila siku wanataka kupata wao tu, wakiona mwingine anaanza kupata watafanya kila mbinu, hata ikibidi wakutoe roho lakini mpaka waone nao wanamega cha mnyonge.

    ReplyDelete
  13. Jamani mbona tunakuwa kama Nduli? Siku zot etulikuwa wapi hadi tuanze k ukurupuka leo.

    ReplyDelete
  14. CNN WAFUNGIWE KAMA MWANAHALISI KWA KUPOTOSHA,KAMA KWELI WAMEPOTOSHA.

    ReplyDelete
  15. Hizi porojo zoote zimefanya nijue na kufikilia kitu fulani! Nionacho mimi kwa mawazo yangu, nimekuja na jibu muafaka kwamba hayo mafuta yapo ziwa nyasa upande wa Tanzania. Yangekua yapo upande wao haya yote yasingetokea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...