DJ Nijo wa Hyped East Africa (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa kutambulisha uzinduzi wa shoo kali itakayofanyika jioni ya leo katika ukumbi wa Club Bilcanas.Kushoto ni DJ Ejay wa Club Bilicanas na kulia ni Fadhilili Mwasyeba Meneja Wa Zuku Tanzaia.
Kipindi maarufu cha “Hyped East Africa Show” kinachorushwa na king'amuzi cha Zuku Pay TV wanaendelea kutafuta klabu bora Afrika Mashariki ambpo leo imemleta DJ Nijo kupiga shoo kali kwenye Ukumbi maarufu wa Club Bilicanas jijini Dar es Salam.
John Waititu a.k.a Dj Nijo alingia jijini Dar es Salaam jana, ijumaa ambapo Jumamosi ya leo atatoa burudani kabambe kwa wakazi wa jiji hili.
Akizungumza na waandishi wa habari, John Waititu a.k.a Dj Nijo alisema “Ninayofuraha kurudi Dar Es Salaam kwaajili ya kuendelea kutafuta klabu bora Afrika Mashariki. Tulivyo tembelea Dar Es Salaam mara ya mwisho, mashabiki walipenda shoo na ndio ilipelekea kurudi tena kwa mara nyingine."
Pia aliongezea “ Jumamosi hii tutakuwa na show ya Saturday Night Fever na tutakuwa na DJ’s Ibra, Paul and Ejay wa Club Bilicanas. Aliwakaribisha watu wote kuja Club Bilicanas kuwakilisha jiji lao, ili ichaguliwe kuwa klabu bora Afrika Mashariki.”
Timu ya Hyped East Africa inategemea kuwaona wasanii wabongo wakihudhulia show hiyo kwa ajili ya kuwafanyia usaili ambao utaonyeshwa kwenye shoo ya Hyped East Africa ya Zuku Afrika.
Akiongea na wandishi wa habari, Fadhili Mwasyeba, Meneja wa Zuku Tanzania alisema ” Zuku inaendelaa kuwekeza nchini Tanzania, na ujio wa Dj Nijo kwa mara ya pili ni moja kati ya ahadi zetu. Na siku ya leo tunataka watu kuja kwa wingi kwajili ya kuwakilisha jiji la Dar es Salaam.”

Aliongezea pia kuwa kwenye shoo hii, kutapambwa na ubora wa hali ya juu na wengi watasuuzika kwa kushuhudia shoo hiyo ambayo imekuwa ikiacha gumzo kila jiji anazopiga shoo DJ Nijo zikiwemo ndani ya Afrika Mashariki. Pia watu watapata nafasi kupiga picha na masupa star na kujishindia zawadi.
DJ Nijo yuko kwenye ziara ya kupiga shoo kwenye klabu maarufu za miji mikubwa ndani ya Afrika Mashariki na vipindi vyote vya Hyped East Africa vinarushwa Zuku Afrika kila jumamosi saa 3:30 usiku.
Shoo ya “Hyped East Africa” imefanywa Kampala (Cayenne Club & Anjenoir (Gavuno) club), Dar es Salaam ( Nyumbani Lounge & Club Sun Cirro), na miji megine 8 hapo Kenya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...