Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imetoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa wanajeshi watatu waliokuwa wakishitakiwa na kesi ya  kumuua mtoto wa Chifu Abdallah Fundikira, Swetu Fundikira kwa kukusudia. Adhabu hiyo imetolewa mapema leo baada ya kuwakuta na hatia washitakiwa wote watatu kwa mashitaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Wanajeshi hao ni Sajenti Rhoda Robert (42) wa  Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Mbweni,Koplo Ally Ngumbe (37) wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) kikosi cha Kunduchi na Koplo Mohamed Rashid. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Zainabu Mruke ambaye alisikiliza kesi hiyo.

Katika hukumu yake Jaji Mruke alisema kuwa imethibitika kuwa washitakiwa waliua kwa kukusudia.

"Midhahir hakukuwa na shahidi wa moja kwa moja washitakiwa waliua lakini mazingira yanaonesha Swetu aliuawa na washitakiwa hao" alisema Jaji Mruke. Aliongezea kuwa ni wazi upande wa mashitaka umeweza kuithibitishia mahakama pasi na shaka yoyote kuwa washitakiwa walitenda kosa la mauaji ya kukusudia.

Marehemu Swetu aliuawa kutokana na majeraha yaliyotokana na kupigwa kitu kichwani, jambo ambalo  lilithibitishwa na Daktari  wa Hospitali ya Taifa Muhimbili aliyetoa ushahidi kuwa alifanyia uchunguzi mwili wa marehemu.

Kwa mujibu wa ushahidi, Januari 23 mwaka huu, Marehemu Swetu alikutana na washitakiwa katika makutano ya barabara ya Kawawa na Mwinjuma Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es salaam,  ambapo baadaye wanajeshi hao walimchukua wakidai kuwa wanampeleka kituo cha polisi cha Oysterbay lakini hawakumpeleka huko. Badala yake  alikutwa usiku wa manane eneo la msikiti wa Jamatini, Upanga, jijini humo, akiwa na washitakiwa katika hali mbaya mpaka mauti yalipomkuta katika hospital ya Taifa ya Muhimbili walikodaiwa kuwa walikuwa wanampeleka.

Hata hivyo hawakufanya hivyo na baadaye walikutwa katika eneo la msikiti wa Jamatini huku mwili wa marehemu ukiwa umelala kifudifudi ukiwa hauna nguo yeyote zaidi ya soksi ya mguu wa kulia ambapo katika utetezi wao walidai kuwa  Swetu alivua nguo mwenyewe na kwamba alijirusha kutoka kwenye gari wakimpeleka kituo cha Polisi Kikuu.

Washitakiwa walishindwa kutoa maelezo ya kutosha kuhusu kifo cha Swetu kwa sababu ni wao ndio waliondoka nae akiwa katika hali ya uzima na ni wao walikutwa nae akiwa hoi hajitambui, na baadaye kufa.

Kama ambavyo inafahamika adhabu ya kunyongwa ni adhabu kubwa, ndugu wa washitakiwa hao walilia mahakamani baada ya kusomwa hukumu hiyo huku wengine wakizimia. 

Hata hivyo wakili wa washitakiwa hao Mhe Ruge Kalori hakuridhishwa na hukumu hiyo  hivyo alisema kuwa atakata  rufaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Haki imetendeka JK nakuomba usaini kunyongwa kwa watu kama hawa!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. yani huyu jaji sijui alikuwa wapi kwa kesi ya mwangosi kwani hawa watu wanaoitwa mapolisi wanajeshi ni waonevu sana kwa rahia wamewekwa ili kulinda raiya, lakini wanafanya kinyume,kweli sheria ipo kwa ajili ya mvunja sheria litakuwa fundisho kwa mapolisi wengine na wanajeshi gooood joooob jaji.

    ReplyDelete
  3. hatufurahii watu kunyongwa, but hili liwe fundisho, na haswa kwa wanajeshi kwa tabia yao ya kupiga watu bila hata sababu za msingi.

    ReplyDelete
  4. Kama hakuna ushahidi wa moja kwa moja nina mashaka sana na hukumu hii. Hukumu ya kifo ni lazima ithibitishwe pasipo shaka!!!

    ReplyDelete
  5. Wakati wanamuua raia asiye na hati walikuwa WALEVI tena WAZINIFU wa mke wa mtu na huyo mwanamke alieolewa anamuongopea mumewe amesafiri kumbe MZINIFU tu mmoja sasa kwenye HUKUMU wamekuwa WASWALIHINA
    Sio mbaya ila ni kutafuta KICHAKA cha KUJIFICHA

    ReplyDelete
  6. Tunawaombea mungu hawasamehe kama kweli walitenda kosa maana ukweli wa tukio shahidi ni watuhumiwa na marehemu.Pole Jaji Mruke kwa kazi nzito.

    By GGEF (T) Traders

    ReplyDelete
  7. Please Mr president naomba uisaini hati ya hawa jamaa kabla hujang'oka madarakani

    ReplyDelete
  8. Daah aisee inaonekana walikuwa wanasali sala 10 kumi kwa siku.... hizo sijida huwezi amini waliua hawa...

    ReplyDelete
  9. Je ni nani anakumbukumbu mara mwisho mtu {raia} alinyongwa tanzania/tanganyika,huyu jaji kabadilisha sheria za nchi au alikuwa anataka umaarufu,hanyongwi mtu hapa,kama nikifungo cha maisha sawa, if there are guilt.Nchi inaendelea tusirudi nyuma watz! we are civilazied society!

    ReplyDelete
  10. KWA THAMANI YA UBINAADAMU TUSINGEPENDA WAHALIFU HAWA WANYONGWE,

    ISIPOKUWA KWA MATENDO MABAYA HAYA HAPA CHINI:

    1.MAUAJI YA MTU ASIYE NA HATIA,
    2.UZINIFU NA MKE WA MTU,

    NI BORA WANYONGWE KWA KUTOA UHAI WA MTU ASIYE NA HATIA NA KUZINI NA MKE WA MTU!!!

    ReplyDelete
  11. Ama kweli za Mwizi ni 40 !

    Jamaa walikuwa 'wanamla' mke wa mtu mwishowe Mwenyezi akawaumbua kwa kufanya mauaji wakiwa na Mke wa mtu na sasa na wao wananyongwa !!!

    ReplyDelete
  12. Kwani ni nini chimbuko la huo ugomvi ulopelekea wakamuuwa huyo kijana?

    ReplyDelete
  13. Ajuaye ni Mwenyezi Mungu:

    Mtihani mkubwa saaana huu, yaani mnafanya Uzinzi weee haitoshi, mnafikia mnafanya mauaji ya kinyama kabisa.

    Hivi kweli kwa akili ya kawaida Maombi yenu yanapokelezeka?, hata kama mmemkosea mtu asingeweza kuwasamehe sembuse iwe yeye Muweza wa yote?

    Uuumini mzuri mngeanza tokea kabla ya kupata janga hili, inawezekana kabisa yasingewakuta na Mungu angewaepusha na hili Inshallah!

    Halafu leo hii mko chini ya Mkono wa Sheria mnakuwa Waswalihina!

    ReplyDelete
  14. Usanii tu hapo sana sana wataenda kufichwa mtwara tuambiwe wamenyongwa..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...