Kiongozi wa Askari magereza, akiwaongoza Sheikh Ponda na wenzake, kutoka mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, baada ya kuahirishwa kwa kesi yao

Kiongozi huyo mwenye msimamo mkali, alifikishwa kwa mara ya pili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na wafuasi wake ambapo hakimu anayesikiliza kesi dhidi yake, Victoria Nongwa, ya kuvamia eneo la Markaz, Chang'ombe jijini Dar es Salaam, ambapo waliharibu  na kuiba mali mbali mbali zenye  thamani ya shilingi milioni 59, madai ambayo washtakiwa wote waliyakanusha. 

Hakimu huyo alikubali kutoa dhamana kwa washtakiwa wote isipokuwa kiongozi huyo ambaye ni mshtakiwa namba 1 kwa madai kuwa bado Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), hajaondoa pingamizi lake la kuzuia dhamana kwa mshtakiwa namba moja. 

Ulinzi katika mahakama hiyo ulikuwa ni mkali na haujawahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni, ambapo pamoja na mambo mengine, palifungwa CCTV Cameras, vifaa vya kugundua vitu vyenye asili ya chuma, polisi wa kutuliza ghasia magereza na wale wa FFU, polisi wa farasi na mbwa, pamoja na askari kanzu waliotapakaa kila kona ya maeneo ya jirani na mahakama hiyo kubwa jijini Dar es Salaam. 

Kikundi kidogo cha wafuasi wa Sheikh Ponda, kilijaribu kuleta rabsha, lakini polisi walitumia busara na kuwaelekeza kilichoamuliwa mahakamani ambapo pamoja na kusuasua kuondoka eneo hilo la mahakama, lakini hatimaye waliondoka huku  polisi wa kutuliza ghasia wakiwafuata kwa nyuma hadi eneo la makutano ya barabara za Bibi Titi na ile ya Morogoro nao wakatawanyika. 

Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika vya habari, kulikuwepo taarifa kuwa wafuasi hao walipanga kutega milipuko kwenye eneo la mahakama na pia walisambaza vipeperushi vyenye vitisho kadhaa, ikiwa ni pamoja na kufanya maandamano makubwa ya kulazimisha kiongozi huyo aachiliwe. 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena


Wafuasi wa Ponda, wanbaoshatakiwa pamoja naye, wakifunguliwa pingu mahakamani
Mshtakiwa akiwa amebebwa na mwenzake baada ya kudondoka mahakamani na kupoteza fahamu
Askari wa kutuliza ghasia magerezani, nao walikuwepo kikamilifu

Askari wa kutuliza ghasia magereza, akiwa ameshika lindo mbele ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Alhamisi Novemba 1, 2012

Polisi wa Mbwa nao walichukua nafasi yao

Huiingii mahakama ya Kisutu bila ya kukaguliwa na mashine za kugundua vitu vya asili ya chuma hapo.
Farasi wa polisi wakiwafukuza wafuasi wachache wa Sheikh Ponda, waliojikusanya nje ya uzio wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Alhamisi Novemba 1, 2012
Polisi wa Mbwa wakisubiri amri ndani ya gari lao nje ya mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Novemba 1, 2012
Polisi wa Mbwa akifanya doria kwenye barabara ya Bitbi Titi mbele ya jengo la mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
Askari Magereza wa kutuliza ghasia, aliyejihami kwa silaha na vifaa vingine akiwa makini kulinda usalama
Sheikh Ponda na pingu zake mikononi, akirejeshwa rumande.

Habari na Picha kwa Hisani ya K-Vis Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Ponda kama hataki kutulia akatafute nchi nyingine akaishi..asitubabahishe.Lazima afuate taratibu za nchi..haya sasa ak*ny** ndoo.

    ReplyDelete
  2. wataanguka sana!!! wenzao wametulia tu wanawaangalia kwenye luninga, waache kimbelembele cha kuandamana bila kujua madhara yake!!

    ReplyDelete
  3. Sheikh mponda inshallah kwa uwezo wa M/mungu utatoka.kwani yote ni mipango ya watu wachache wasiopenda wailsamu waendeshe mambo yao bila ya amani.

    Kwani wenzetu wadini zingine hata wakiuwa au kufanya biashara za unga hawadhalilishwi kama waislam.

    ReplyDelete
  4. Wewe mdau wa Thu Nov 01, 08:23:00 PM 2012, hebu funguka macho na akili ndugu yangu. Hakuna uislamu wala chochote, walichofanya shehe Ponda na wenzie wala si uislamu, bali ni vurugu ambazo zinahatarisha hali ya amani nchini. Ndugu yangu wewe huoni wenzetu wanavyopata shida nchi za wenzetu wakiuana wenyewe kwa wenyewe. Chanzo ni kuachia mambo kama haya ya kujenga chuki zisizo na msingi za kidini ama kikabila. Mimi ni muislamu kama wewe lakini siamini hata kidogo kama njia waliyotumia shehe Ponda na wenzie ni sahihi. Tutunze amani yetu jamani. Dini hizi zisituwekee matabaka. Waislamu kwa wakiristo tumezaliana na tumekuwa tunashirikiana bega kwa bega. Sasa ukianza kujenga matabaka ya udini utaanzia wapi ndugu yangu?. Sisi ni watanzania kwa kuanzia, hebu tuutunze utaifa wetu. Hebu kaa chini tena tafakari..

    ReplyDelete
  5. laiti kama hao kina Ponda wangelikua na fikra, upeo na mtazamo kama wa mdau huyo juu hapo (Nov 1, Thurs 11:00:00PM 2012)..muda na rasilimali nyingi zaidi taifa hili zisingepotea bure kwa ajili ya kuwalinda watu wachache wenye matakwa yao binafsi, yasiyo na tija kwa jamii ya kitanzania.
    "NAAMINI KWAMBA BINADAMU WOTE NI NDUGU ZANGU NA AFRIKA NI MOJA"..
    MUNGU ibariki Afrika,
    MUNGU ibariki Tanzania, Amen.

    ReplyDelete
  6. mpaka Leo mnakalia nyumba za udongo mkitetewa ohhh ponda hivi ponda vile. sisi wa mbagala tunataka haki yetu tulinyanganywa na baba yenu mkapewa nyinyi wa masaki. tetea wanyonge ponda mlipaji mungu. mimi nihesabu kwako.

    ReplyDelete
  7. Jambo la msingi la kukumbuka Nikwamba wote tumetoka kwa baba mimoja,Abraham. Mengine ni yakujitengenezea. Our own making

    ReplyDelete
  8. Haya matatizo yote yanatokea kwasababu Serekali inafungia macho mambo wanayo dai Waislam hata yawe na ukweli kiasi gani. Kwamfani
    1..Swala lamatokeo ya mitihani namna yalivyo chakachuliwa na mpaka leo wahusika hawaja wajibishwa.
    2..Hicho kilicho chukuliwa ni kiwanja cha waislam sasa mbona huyo anae ona kadhulumiwa kiwanja chake hendi kushitaki yeye, kwani kuna kesi ngapi zaviwanja vilivyo vamiwa mbonna watu hawashikwi na mtutu wabunduki

    ReplyDelete
  9. Vipi mbona Ponda hajanyolewa ndevu kama mwenzie wa Unguja? au kule ni Chuo Cha Mafunzo na huku bara ni Magereza?

    ReplyDelete
  10. Wewe mdau wa 8:32 PM nafikiri una shida sana ya kufikiri, Unaona ni sawa huyo unayemwita sheikh alete fujo na kuumiza wengine na unaona pia ni haki akiua ni sawa tu kwa sababu mkuki kwa nguruwe kwa binadamu uchungu. Jifunze kuwa mtu mzima angalau uwe na akili kidogo tu. Kuchoma nyumba yoyote iwe ya mtu au ya ibada adhabu yake ni kifungo cha maisha jela. Hao kina Ponda siku zote wamekuwa wakibebwa bebwa leo yamewakuta...nina imani safari hii watakoma.

    ReplyDelete
  11. Insha Allah mwenyezi mungu atakusaidia utoke uendelee na uhalifu wako...

    ReplyDelete
  12. SERIKALI INATAKIWA KUWADHIBITI HAWA WANAOTAKA KULETA FUJO KWA KISINGIZIO CHA DINI.WAFUATE TARATIBU ZA KUPELEKA HOJA ZAO KWA VYOMBO HUSIKA.HAWA NI WACHOCHEZI HAWANA HOJA YA MSINGI.WAPELEKWE NGWALA CHUNYA WAKAKATE MBAO.

    ReplyDelete
  13. Fujo za aina yoyote ile tujitahidi tuepuke.Kwani zitakapoanza imagine watoto watapotezana na wazazi,hapatakuwa na shughuli zozote za maana zaidi ya kupigana.Mi siamini kama uislamu ndo unasema hivi.Hapa kuna suala la maslahi zaidi.Naambiwa na washikaji kwamba huyu aliyeuziwa hapa kwenye hivi vi eka 4 kanunulia bakwata zaidi ya eka hamsini nje ya mji ili kujenga chuo.Kwenye Eka nne utajenga chuo cha namna gani ?mbona hilo halisemwi ?Halafu huyu mshitakiwa wa kwanza tunaambiwa kwamba ni raia wa burundi na aliwahi fukuzwa Tanzania.Nani kamruhusu kama tayari alishapewa personal non granta ?

    ReplyDelete
  14. HUYO AFANDE MWENYE NYOTA MBILI PICHA YA KWANZA JUU ALIE MBELE YA MWANAHARAKATI PONDA HUWA ANAIGIZAIGIZA MOVIES HASA ZA J PLUS KAMA MKUU WA MANJAGU KUMBE NIKWELI NI MKUU WA MARAS MAKUNJA?...

    ReplyDelete
  15. Ndg zangu elimu yetu Waislamu ni duni sana. Tunakosa hata kufikiri vizuri na kuwaza mambo mabaya eti wote tukose. Tunajiingiza katika mambo ambayo yatatuletea matatizo. Naomba mjiulize mmoja mmoja hapo rumande kuhusu elimu mlio nayo. Acheni kutuaibisha kiasi hicho. Heshimu walio madarakani-period!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  16. Serikali imewalegezea kitambo sasa inatumia nguvu zaidi kuwanyoosha, samaki mkunje angali mbichi. Cheki kijana mdogo kazimia sababu ya kufuata mkumbo, ponda kwao burundi wamezoea mtanange, wewe je?

    ReplyDelete
  17. TATIZO WAKATI MWINGINE SISI WENYEWE NDIO TUNAOUKUZA HUU UDINI MAANA NAONA KILA MTU HUMU ANAKOMENTI KIDINIDINI TU...KAMA MMEFUATILIA KWA UMAKINI ISHU YA SHEIKH PONDA HAIHUSIANI NA VURUGU ZA KIDINI DHIDI YA NDUGU ZETU WAKRISTO...BALI NI MGOGORO WA KUUZWA KIWANJA CHA WAISLAMU KINYEMELA ULIOFANYWA NA VIONGOZI WENYE NJAA WA BAKWATA..TUSIHUSISHE SUALA HILI NA UDINI JAMANI.HAKUNA UDINI HAPA OTHERWISE KAMA MNAMTETEA MNUNUZI KWAKUA NI MKRISTU??...HII NCHI IMEANZA KUNCHEFUA.BORA NIJIRUDIE RWANDA MAANA YALE YA 1994 NAHISI YANATAKA KUHAMIA HUKU....KWAKWELI MKOLONI KAONDOKA LAKINI KATUACHIA JINAMIZI BAYA SANA...

    by MCHANGIAPOTE...

    ReplyDelete
  18. Jamani asili ya shehe Ponda, ni wapi? tukiachana na haya mambo ya udini, niliona mesage mmoja inasema asili yake ni burundi? ni kweli, kama ni kweli hmmmm, basi ni kawaida kwa kupenda vita na kumwagana damu za binadamu wenzao, manake huko burundi au Rwanda vita ni kawaida kwao, na vita ni kumwaga damu za binadamu wenzako, alafu kwa kuwa wewe ni kiongozi haaa unapeta tu wala madhala hayakufiki, na viata ni vita iwe ya dini au kikabila au Taifa hmmmm ni vita, hapo chacha, Mungu linusuru Taifa hili na haya majanga, ya binadamu wachache wanopenda mwaga damu za wenzao

    ReplyDelete
  19. mimi ni mwislam safi na nasikitika kusema kwamba waislam tumezidi fujo kha, hadi natamani nibatizwe tu

    ReplyDelete

  20. Mungu atupe subira sheikh Ponda. In shaa Allah madua yetu yatapokelewa.

    ReplyDelete

  21. Mengi yamekuja na kupita, Ponda alishawahi kuambiwa ameingiza makontena ya majambia.
    Mengi yatasemwa, iko siku, fitna huwa ina mwisho.

    ReplyDelete

  22. Huyu mtu ku##ea ndoo sio tatizo, yeye pamoja na wenzake ni watu wenye akili zao timamu isipokuwa mnyonge huwa hana haki, wachangiaji wengi wako na mtizamo hasi dhidi ya hawa jamaa.
    Fuatilieni kwa kina mtagundua hawa jamaa wako sawa.
    Mbwembwe za hao wajomba kama wako vitani zisikuchoteni akili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...