Assalam aleykum kaka Issa Michuzi, 
Mimi ni blogger kutoka huku ng'ambo, nazungumzia visiwani Zanzibar, ila hasa hasa Pemba, namanisha mpemba halisi.
Kupitia libeneke lako naomba namie kulitambulisha libeneke langu ambalo linasomeka kwa anuani hii 
Napenda kuitambulisha kwa wanajamii ili kupata ushauri wao juu ya fani au sanaa hii.
Ahsante.
Natanguliza shukrani.
Mwanalibeneke Pemba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Wapemba wakiiyona hii blog yako watakumwagia tindi kali!!

    ReplyDelete
  2. Ndugu yangu wazo lako lauanzisha blog ni zuri, lakini nimetembelea hiyo blog yako na nimeona yafuatayo.

    1. Umeshindwa kutumia bahati ya kuepo sehemu tofuati na wanablog wengi badalada yake umekuwa una unaendesha blog yako kama wafanyavyo hao wengine... Una copy na ku paste kutoka mitandao mengine! Hakuna jipya

    2. Hakuna ubinifu wowote!

    Ushauri: Kwavile una blog ukiwa PEMBA ungekuwa unaweka matukio na picha nyingi zaidi ya matukio ya huko Pemba au Zanzibar kwa ujumla. Hii ingekutofautisha na blog nyengine nyingi. Na pengine ungekuwa source ya habari ya blog nyengine kujuwa yanayotokea Pemba na Zanzibar kwa ujumla! Ila kwa mwendo wako huu wakuweka picha za ku copy hautafika popote.

    Imagine uko zanzibar lakini kwenye blog yako hakuna picha wala habari hata moja ya yanayotokea zanzibar, si ya kisiasa, burudani wala maisha ya kawaida. Utafkiri una blog ukiwa USA maana kumejaa picha za akina NICK MINAJ!

    ReplyDelete
  3. Karibu Mwanalibeneke mpya na tunaomba zaidi ya yoooote uulinde MUUNGANO!

    Kama Muungano ukifa je itakuwaje,

    1.Klabu za Yanga SC na Simba SC tutazipanga vipi maana pana wanachama wake na wapenzi Bara na Visiwani?.

    2.Chama cha Mapinduzi tutakigawa vipi maana kina wapenzi na wanachama Bara na Visiwani?.

    3.Chama cha Wananchi CUF kina wapenzi na wanachama Bara na Visiwani tutakigawa vipi?.

    4.Watu tumeoleana na kuzaliana kwa mseto Bara na Visiwani tutapanga vipi na kugawa koo na familia zetu?

    5.KUBWA LAO:
    Wakati mwingine waungwana wanalazimika kusafiri na kuja Bara ili kula neema hizi mbili hapa chini:

    (i)Pana yele majani ambayo ni dawa 'ganja' yana wapenzi na watumiaji Bara na Visiwani hadi Pemba kwa Masheikh tutagawa vipi hapa?

    (ii)Pana maji ya 'Konyagi-B' a.k.a Gongo hata Masheikh wanakata maji kimtindo kwa kujificha tutagawa vipi hapa?

    TUNAOMBA BUSARA ZAIDI NI VIGUMU KWA POINTI HIZO 5 HAPO JUU KUUVUNJA MUUNGANO!!!

    ReplyDelete
  4. Hahahahahaha!!!

    Mtoa Maoni Anonymous wa 3 wa Mon Nov 12, 10:55:00 AM 2012

    ...Pana jaamaa walisafiri kwenda Pemba kwa kazi za Ujenzi wa Majumba, walipofika Mwenyeji wao alikuwa ni Muungwana akawatahadharisha ya kuwa watu watakao onana nao (wenyeji) akijua kuwa watakwenda ktk sehemu za Pombe haramu ya Gongo wasikubali kupewa trakrima!!!

    Jamaa aliposema hivyo walishangaa kwa nini?, yeye akiwasisitizia kuwa wasikubali ni vile kule mgeni akilewa akaangusha gari basi anavunjiwa 'bucha' lake na wenyeji walio mkirimu Gongo hilo!!!

    ReplyDelete
  5. Mdau wa Tatu kila sehemu ina neema zake maana maisha yamegawanyika!

    Zanzibar na Pemba pana Karafuu, ila mengi yanayopatina Bara Visiwani ni adimu na yanayopatikana Visiwani Bara ni adimu.

    Moja ya burudani zinazofuatwa na Waungwana wa Visiwani wanapokuja Bara licha ya neema zingine hizo ulizozitaja kibao ni 'akina dada wa usiku' a.k.a Machangu !!!

    ReplyDelete
  6. ahsanteni sana kwa maoni na ushauri wenu , inshallah ntaufanyia kazi na suala la muungano musjali kwa kuwatoa khofu inshallah tutaulinda kwa nguvu moja.
    by: CEO Kakytee Blog

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...