Nilitoa tangazo kuwa kijana mmoja wa kisomali anautafuta ukoo wake na nilifanikiwa kukutana na mhusika mmoja ambapo alikuja nyumbani na kumweleza kila kitu pamoja na mahali alipo huyo kijana na aliaidi kumpelekea ujumbe huo muhusika mkuu anayeitwa HUSEIN ALLLY mkazi wa makuyuni ,arusha ambaye ndiye baba wa huyo kijana.
Cha ajabu ni kwamba mpaka sasa mzazi huyo hajatokea wala kufanya mawasiliano yoyote na sisi mana tulimweleza kuwa asiwe na wasiwasi na sisi ili akamchukue mtoto wake kwani anaishi katika mazingira magumu mno .
Nawaomba ndugu zangu wasomali msiwe na roho za kikatili kwa kuwatenga watoto wenu mliozaa nje ya ndoa kwa wanawake wasio wasomali. Namuimiza sana huyo mzee HUSEIN ALLY akamchukue mtoto wake tulipomwelekeza alipo mana damu ni nzito kiliko maji.
Mdau Makuyuni, Arusha
mdau kazi umeipitisha na wajibu wako umeufanya mwenyezi mungu atakulipa kila la kheri
ReplyDeletetwengepata watu kama nyinyi mwenye moyo na imani hii mzuri basi hii dunia ingekuwa ndio pepo
ila usijali mungu atakulipa na utaongezewa barka kwenye mihangaiko yako ndugu yangu kuanzia kesho ishallah utakuta mambo yako yanazidi kuwa mazuri kwa wema wako nakutakia usiku mwema
Unataka kuniambia watanzania hawana tabia hiyo? Acha ubaguzi, ongelea tabia, sio kabila! hao watoto wanaotupwa majalalani kila kukicha ni wakisomali?
ReplyDeleteKatika Imani ya kiislamu huyo si mtoto wake,(mtoto wa nje ya ndoa ni mtoto wa mama) hivyo hapaswi kulazimishwa kwenda kumchukua, tena kwenye vyombo vya habari kama hivi. Pili ume-generalize kwamba eti wasomali waache roho za ukatili za kutupa watoto, sio kweli wasomali hawana tabia hiyo bali hiyo ni Tabia ya mtu.Hata wewe unaweza ukawa nayo.
ReplyDeleteKama ujumbe atakuwa kaupata basi vuta subira anaweza kufanya hisani ya kuja kumchukua huyo mtoto na kumlea na sio kumlazimisha kumchukua. Hili ni jambo la ghafla na pengine anahitaji kujipanga kabla ya kufanya hiyo hisani.
Ni hayo tu.
Mdau Kisiju Pwani.
kwa akili yako ukibandika post na kashfa ndo atafanya?
ReplyDeletejifunze kuwa na lugha nzuri inayofanya malengo yako yatimie.
mpaka umejuwa kutembelea blog lakini hujajua kauli njema.
Kwa kweli Huna busara kabisa utawachanganya Vp wasomali Wote Kwa swala hili unataka kuniambia hao watoto wanao omba omba Kila kona ya hiyo nchi Ni wasomali? Think before you talk, do a DNA test ndio uongee unasema kama Huna kichwa. Watu kama wewe ndio wanao anzishaga vurugu ktk nchi.
ReplyDeletefrom the negative posts above utajua tuu hao wote ni wasomali.
ReplyDeleteKwa hiyo tumsifie kwa kumtupa mwanae?!! au tumseme na kukemea hii tabia?
bahati mbaya, tabia za wasomali wengi zinajulikana! huhitaji darubini wala DNA kujua.
Shida sana... sijui tutafika lini?
Huyo alosema mtoto aw nje ya ndoa ni mtoto wa mama since when?usisingizie Imani tumia akili yako maana hiyo Imani pia inakataza zinaa nae kazini na mwanamke asiyefunga nae ndoa,maji yashamwagika,mtoto kashazaliwa Hana hata kosa,huyo jamaa achukue kiumbe wake kuliko mtoto aendelee kumangamanga mtaani,na mtoa taarifa kasisitizia swala la usomali kwasababu kidesturi wasomali hawaoani na waswahili ni nadra siyo common kuona couple za kisomali +kiswahili naamini Hana nia mbaya.Hata hivyo Kama tungejitahidi kuchukua watoto tunaowazaa nje ya ndoa na kuwapa elimu bora na malezi bora naamini watoto hao wangekuwa na maisha mazuri na ya furaha,kwanini tuache watoto wetu wakitaabika bila elimu,upendo,malezi bora ilhali ni wetu hata Kama tumewazaa nje ya ndoa,tuwachukue Hawana hatia hao,kosa ni letu sie wazazi
ReplyDeleteMtu kama huna point yeyote ya maana ya kuzungumzia ni bora uweke maoni yako na hisia zako mbali na mjadala. Huwezi kuropoka tuu mradi umezungumza. Sasa huyu bwana anaedai hao wote waliopinga kauli ya kujumuisha wasomali wote ni wasomali and they are negative. Unaposema tabia za wasomali wengi zinajulikana!. Huoni kwamba unajumuisha jamii nzima na wewe mwenyewe una-sound so negatively. Na pia unakuwa umetoka njee ya mada kwa kuingiza hisia zako kwa kudai eti unazijua tabia za wasomali wengi kwani jamii nzima walikutia mimba wewe na kukuacha msele mpaka ukazijua tabia zao?.Hapa unatakiwa uchangie jinsi ya kumsaidia au kuwwawezesha huyo kijana na huyu mzazi alieshindwa kutimiza wajibu wake kuwa pamoja au jinsi ya kumsaidia huyo mtoto. Sio uendeleze misjudgements and negativity by painting the whole community badly. Watu kama wewe na huyu mdau wa Makuyuni wenye upeo finyu wa kimawazo kwa kudai kosa la mtu au watu wachache basi unahukumu jamii nzima ndivyo ilivyo. Mnakosea na mnatakiwa mfikirie kabla hujasema au hujaandika.
ReplyDeleteBy the way mii sio msomali!
Baba wa mtoto Hussein Ally alikuwa na azma njema ya kuoanana na mwanae alipopewa taarifa isipokuwa alipangwa kujiunga na Wapiganaji wa AL SHABAAB na sasa yupo Somalia huku wakiwa wamezingirwa na Majeshi ya Serikali ya Somalia (Somali National Ermy-SNA) !
ReplyDeleteSasa wandugu atachomoka vipi huko Somalia ili kurudi hapo Mombo/Makuyuni-Tanzania kwa mwanaye?
I know have seen this post 4 years letter , Mi msomali mkenya na utu hauna kabila.
ReplyDeleteAli Hussein a-take responsibility!