Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Janeth Mbene akitoa hotuba yake wakati wa Uzinduzi wa Kampuni ya Bima ya Afya ya Resolution katika hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Uzinduzi wa Kampuni hiyo umekuja rasmi mara baada ya kupata cheti cha usajili wa kutoa bima ya afya nchini kutoka kwa Mamlaka ya Usimamizi ya Bima (TIRA).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bima ya Resolution,Peter Nduati akizungumza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa Kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam hivi karibuni,ambapo alisema kuwa Kampuni yake imejipanga kufanya mapinduzi katika soko la Tanzania.
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Israel Kamuzora akizungumza kwenye hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Janeth Mbenr (kushoto) akiwa pamoja na Mjunbe wa Bodi ya Kampuni ya Resolution,Richard Kasesela wakati wakifuatilia kwa makini taarifa fupi iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bima ya Resolution,Peter Nduati (hayupo pichani).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Richard Kasesela huyu nae mjumbe katika kila bodi hivi hakuna watu wengine au ndio usalama wa taifa lazima muwepo kila sehemu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...