Halmashauri Kuu ya Taifa ya CHAMA CHA MAPINDUZI  CCM iliyokaa kikao chake jana tarehe 10 November 2012, imependekeza jina la Ndugu. Phillip Mangula (pichani) kuwania nafasi ya  Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara huku Rais wa Zanzibar Mweneyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar,Dk. Ali Mohamed Shein akipendekezwa kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Kizota Mjini Dodoma,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kuwa majina hayo yatapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu siku ya jumanne.

Hata hivyo ndugu Nape, amewaambia waandishi wa habari kuwa kikao cha NEC kimepitisha kwa kishindo jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti CCM Taifa.

Pia kikao cha NEC kimefanya Mabadiliko kidogo ambapo leo tarehe 11 Novemba wajumbe wa NEC nafasi kumi bara na kumi Zanzibar watapigiwa kura badala ya kesho, na matokeo yatatangazwa mara baada ya uchaguzi kumalizika.Wajumbe wote wa mkutano kutoka mikoa yote wameshawasili Mjini Dodoma tayari.

Wakati huo huo Rais Jakaya Kikwete kabla ya kufungua mkutano mkuu ataweka jiwe la msingi la Makao Makuu mapya ya CCM eneo la Makulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...