Mnyonge mnyongeni, ila haki yake mpeni. Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam Mstahiki Jerry Silaa anastahili pongezi kwa juhudi zake za kulifanya jiji hilo kuwa safi na la kijani. Tayari mizunguko yote ya katikati ya jiji imefanyiwa ukarabati na kuwekewa nakshi kama inavyoonesha pichani. Lakini pamoja na yote hayo wakaazi wengi wa jiji hilo wamemtaka Meya huyo kijana na mchapakazi atupie jicho bustani ya Mnazi Mmoja garden ambayo kwa sasa imefungwa na haitumiki na walipa kodi hadi kuwepo na shughuli maalumu.
Wakaazi hao wamemuomba Meya wao awarejeshee mabembea na vifaa vingine vya kuchezea watoto, afungue kufuli katuika mnara wa saa ili wananchi wapate kuingia, wakisisitiza kwamba kisababu cha wananchi kutokuwa wasafi haileti mantiki kwani Dar es salaam ni jiji pekee duniani ambalo 'Central Park' yake hagusi mtu. Wameongezea kwamba askari wa jiji ambao kazi yao kuu inaelekea ni kufungia magari yaliyopaki vibaya na kutimuana na wamachinga na mama Lishe kila kukicha, wapangwe bustanini hapo kuangalia usalama. Mstahiki Meya Jerry Silaa upo hapo??


Kiingereza hicho anawaambia Wazaramo au Wazungu?
ReplyDeleteKazi kweli kweli!
ReplyDeleteIsiishie kwenye bustani tuu, hilo jengo hapo linahitaji 'facelift' pia...
Halafu bango halikuwa na ulazima wa kuwekwa hapo, mheshimiwa KEENJA miaka hiyo alikuja na wazo zuri sana la kupanda miti, mheshimiwa MAKAMBA pia alikuja na wazo la upandaji miti akisisitiza miti ya matunda tupate kivuli na matunda.
Sasa huyu kaja na bango, sijawahi kuona meya kwenye bango.
Mhe.Meya Slaa,
ReplyDeleteKATA KATA KATAA KUIFUNGUA BUSTANI YA MNAZI MMOJA LABDA KAMA KUTAKUWA NA ULINZI SHIRIKISHI SAWA.
TATIZO NI KWA NDUGU ZETU WA 'KETE' NA 'MATEJA' WATAFANYA NDIO MASKANI YAO.
TATIZO LINGINE WATAKUWA WATU WA MAKUNDI MENGINE KAMA MAKAHABA NA OMBA OMBA (WATAJISAIDIA HIVYO HAPO) AMBAO WATAPATUMIA VIBAYA NA KUWA FEDHEHA !!!