Pamoja na kwamba Serikali imekuwa ikikemea sana swala la ukataji miti nchini,lakini bado somo hilo limekuwa ni kitendawili kwa baadhi ya wakazi wa vijijini,ambao wao wamekuwa wakiamini kuwa Mkaa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu hivyo ni lazima utumike.je nini kifanyike ili kuwafanya watu hawa wasichome miti hovyo na kuaminishwa kuwa bila mkaa wanaweza kuishi??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Tatizo ni wakazi wa mijini. 99% ya wakazi wa mijini wanategemea mkaa kama nishati kuu ya kupikia. Mbaya zaidi hata viongozi na maafisa wakubwa, ukienda kwenye majiko yako lazima utakuta mkaa. Mijini mkiacha kutumia mkaa, mtasaidia sana.

    ReplyDelete
  2. Simple solution
    Give them another and cheap source of energy
    What else can they use for cooking etc.Watu wametumia mkaa maisha yao yote na hapo kwetu vijijini hakuna njia nyingine ya kupika na kusonga, ukiondoa mkaa, kuni na vifuu..Serikali ianzishe mpango wa matumizi ya gas for cooking kama kule Uarabuni. Niliwahi kusoma juu ya matumizi ya mwanga wa jua kwa mapishi kule Kenya, does anyone know about this? Tuelimishe.

    ReplyDelete
  3. hapo najuwa lengo lako ni kumchongea huyu jamaa kwa mali asili ili azidi kuteseka na maisha na ashindwe kabisa na mdudu njaa

    kwa taarifa hii ulieleta hii habari ushindwe na uregee

    ReplyDelete
  4. Mbadala wa mkaa kama nishati ni upi? Wanyonge wengi hupika kwa kuni na mkaa. Hata wenye hali nzuri ya kiuchumi hawataki kutumia umeme kwa kupikia japokuwa umeme ndio nishati rahisi kuliko zote. Hivyo wananchi wanatakiwa wapewe mbadala, mfano vibatari vibadilishwe na taa za solar, gesi ya kwetu (LNG)ipakiwe na kuuzwa kwa bei nzuri, wachache watakaoendelea kukata mkaa wawe na vitalu vya miti waliyoiotesha kufidia watakayoikata.

    ReplyDelete
  5. Huyu mdau anatakiwa awezeshwe kwa kupatiwa mtaji wa kununua gari au pikipiki ya miguu mitatu. Inaweza kujituma na kulipa deni lake.

    ReplyDelete
  6. Wewe ulitaka uingizwe SHAMBA? mkaa ni mjini na kuni ni kijijini!

    Mbadala wa mkaa au kuni ninini? je Serikali imeshafanya juhudi za makusudi ili watu waachane na mkaa au kuni?

    ReplyDelete
  7. Hakuna sababu ya kuendelea kuharibu Mazingira yetu kwa bei ngumu kabisa ya kuyarudisha upya ilihali nchi imeshapata Gesi asilia (LNG).

    La muhimu ni kufanya mipango Benki ya Dunia na Mashirikisho ya Kuiwezeshaji ili kufunga Miundo mbinu na kuanza kuivuna Gesi kwa matumizi yetu na mauzo ili kuongeza kipato cha nchi.

    Raisi wetu JK baada ya mipango ya kuimarisha barabara nchini tafadhali zingatia hili!

    ReplyDelete
  8. Ukisikia kula kwa tindo ndio kupitia kazi kama hizi!

    Halafu angalieni maajabu mtu anavuja jasho kwa kazi kama hii(CHEKI MAGUNIA YENYE LUMBESA MAWILI JUU YA BAISKELI HALAFU KWENYE MLIMA MKALI HUKU JAMAA KIDUME AKIWA MIGUU PEKU PEKU JUA KALI MCHANA LIKIWAKA ANAUNGUA MIGUUNI) anapata pesa zake kwa tabu halafu leo wewe Longo longo unamzima hela zake, kweli patakuwa salama?

    ReplyDelete
  9. Duhhh Ankali!

    Picha za namna hii zingatia usizirushe mara kwa mara zitawatia woga wa Majuu kurudi Bongo moja kwa moja kama kila siku tunavyo wasisitizia, wakiogopa kuja kupata tabu kwa kazi kama hii ya kukata mkaa Kaliuwa-Tabora!

    Jaribu kurusha picha kama zile Raisi Jakaya Kikwete anafungua Mradi wa Gesi pale Kinyerezi ili waone mambo waa ndani ya Bongo!

    Jamaa ndugu zetu Majuu ni waoga sana wa shida na changamoto ktk maisha.

    Watafikiri hizi ndio kazi zetu Wabongo wote huku Tanzania, kumbe wala sivyo kila mmoja na kazi yake wajameni!!!

    ReplyDelete
  10. Hahahahaha!

    Mdau wa 9 tena wa Majuu waambiwe kuwa huyo jamaa yupo Kijijini huko sio karibu na Mjini kwa kuwa siku hizi sio kama zamani barabara za lami ni hadi Kijijini!

    Ama sivyo ile azma yetu ya kuwashawishi wandugu kurudi nyumbani itayeyuka kwa mapicha kama haya.

    ReplyDelete
  11. Msiwalaumu wa Majuu kuogopa kazi ngumu kama ya kukata mkaa mkumbuke ya kuwa hakuna Komandoo wa shida na pia hakuna Bingwa wa shida!

    ReplyDelete
  12. Pana kila sababu ya kubadili mwelekeo ktk matumizi ya mikaa kuachana nayo.

    Gharama kubwa za kuyarejesha mazingira kama awali ni ngumu kumudu pale tukifikia hali ngumu zaidi!

    ReplyDelete
  13. Shughuli peve kama hii ya kukata mkaa na kukokota usafiri wa baiskeli kilometa kwa kilometa kupeleka mauzo Mijini sio rahisi mtu ukaugua visukari na presha!

    Mafuta ya ziada na sukari vinatoka kipitia njia ya jasho.

    ReplyDelete
  14. Mdau anonymous wa Tue Nov 06, 12:09:00 PM 2012

    Naanza na wimbo wa Tshimanga Asossa,

    1.Nilipoanza nayee ,mtu mmwenye alikuwa maarufu sana aaaaaa x3

    2.Toka Ilala sina cheo jamani, mawazo yakanituma niishi pekee aaaaa x 2

    3.Matatizo chungu mzima iyelele mawoo, Mungu kanisaidia iyelele mawoo x 1

    4.Mungu hamtupi kiumbe chake iyelele mawoo x 1

    5.Jamani leo ni kama ndoto ooo yuko mikoni mwangu, iyelele ,iyelele ,iyelele yuko mikononi mwangu x 3 !!!

    Ni muhimu wandugu zetu Majuu watolewe wasiwasi ya kuwa kwa sasa Tanzania hatuna shida kivile TUMEPEWA PROMOSHENI KAMA WIMBO WA TSHIMANGA ASOSSA, NA SASA MAMBO YEEE TUPO WA KWANZA !

    ReplyDelete
  15. Tubadilke Kijamii !

    Imefika wakati watu kama kijana huyu rijali mkata mkaa ndio wa kumwozesha Binti na sio Sharo baro.

    Mfano yule dada aliyekuwa anapitisha bakuli kuomba bia Bar kwa njia ya meseji kwenye karatasi Sinza sio wa kuhangaika ni wa kuolewa na Kidume huyu mkata mkaa!

    ReplyDelete
  16. Mafisadi wanakula neema Vijijini wanakula joto ya jiwe kama kidume hapa!

    ReplyDelete
  17. kazi kama hizi za kukata mkaa ndio kipimo cha urijali !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...