Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akizungumza na Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband wakati ujumbe wa TTB ulipotembelea Uwanja wa Sunderland FC na kushuhudia mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya timu hiyo na timu ya Aston Villa uliofanyika siku ya jumamosi nchini Uingereza, Bodi ya utalii Tanzania inatangaza matangazo ya utalii wa Tanzania katika viwanja sita vinavyotumika kuchezea ligi kuu ya Uingereza (Premier Liegue) kikiwemo kiwanja cha Sunderland FC, katika picha katikati ni Edmund Hazal Mkurugenzi wa Kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo hayo,Bw. David Miliband pia ni mwenyekti wa klabu ya Sunderland.Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani na maafisa wa timu ya Sunderland FC baada ya kukabidhiwa zawadi ya saa kutoka kulia ni Balozi wa Sunderland na Golikipa wa zamani Jimmy Montgomery, Gary Mutchinson Mkurugenzi wa Biashara na Kevin Ball Nahodha wa zamani wa timu hiyo. Balozi wa Sunderland na Golikipa wa zamani Jimmy Montgomery kiutambulisha ujumbe wmaafisa wa bodi ya utalii TTB ulipotembelea uwanja huo.
Ujumbe wa bodi ya Utalii Tanzania ukishuhudia mchezo huo.
Meneja masoko wa Bodo ya Utalii akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hiyo Devotha Mdachi wakati walipotembelea uwanjani hapo jumamosi iliyopita , katikati ni Bw. Mukhtar wa (EAC) nBw. Manase kutoka hifadhi Ngorongoro.
Matangazo ya Utalii wa Tanzania yakipita katika lininga maalum za matangazo uwanjani hapo kama yanavyoonekana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. kaka Michuzi na wadau wa libeneke la Blog ya jamii Salaam.
    Ama kwa hakika huu ni mradi wa kunufaisha watu binafsi kuliko kuleta tija na manufaa katika kuongeza watalii nchini. Wenzetu Kenya badala ya kupoteza hivi pesa wanajenga Uwanja wa Ndege karibu na kwetu ili waweze kuwapata watalii wengi zaidi haswa wenye nia ya kutembelea vivutio vilivyopo nchini mwetu. Wakati umefika kuivunja hii Bodi na Kuiunda upya katika mfumo utakaoleta Tija

    ReplyDelete
  2. viva TANZANIA viva .... ni kazi ngumu lakini mumeanza kwa kishindo,hongereni sana bodi ya Utalii. msichoke kuweni wavumbuzi wa njia nyengine ya Kujitangaza! Hakikisheni maonyesho yoyote ya dunia mnakuwepo kikazi zaidi.Hakuna lisilowezekana,Kwann taifa jirani wapige hatua ya utalii sisi tushindwe? Kazeni buti msichoke TTB

    ReplyDelete
  3. Hongera bodi,hii ndiyo njia muafaka ya kuweza kupampana na "Jirani zetu" baada ya kushindwa kujitanganza kwa kutumia michezo.Kumbe tufanye nini?.Jirani zetu walianza siku nyingi ila hatujachelewa.Haya matangazo ni gharama kweli kweli lakini YANALIPA(Payback).Kama bajeti inaruhusu ilete hiyo timu nchi itembelee na vivutio,na kucheza michezo miwili hivi.Mungu Ibariki Tanzania.

    David V

    ReplyDelete
  4. Mbona Zanzibar hamuitangazi? Waingereza wanapenda kwenda kwenye sehemu za joto kuota jua sio kupanda milima na kutiza wanyama.

    ReplyDelete
  5. Hongereni Bodi ya Utalii kwa hatua hiyo nzuri. Pia nashauri mtumie mashirika ya Ndege makubwa yanayotua KIA na Dar es salaam. Mfano ni kama vile Emirates wanapokaribia kutua katika Airport yao ya Dubai, huonesha video za sehemu za Utalii za nchi yao, ili kuwavutia wageni. Tunavyo vivutio vingi na vizuri sana hapa nchini, ambavyo naamini vikitangazwa katika ndege kubwa ziingiazo nchini itasaidia pia kuvutia watalii. All the best TTB....

    ReplyDelete
  6. kaka unaeuliza kuhusu Zanzibar, si lipo tangazo la "Tanzania land of kilimanjaro and Zanzibar" . Labda uulize hii ni Bodi ya Utalii Tanzania mbona hakuna Mzenji hata chembe au hakuna anaweza kuvaa suti na kusafiri?

    ReplyDelete
  7. Jamaa ubalozi wa TZ.Washington DC ni wababaishaji sana. Naishauri serikali ijue kwamba wabongo walioko ughaibuni ndiyo watangazaji wao wakubwa. Wangekuwa wanawekeza hizo pesa kwenye vyama(vikundi) vya waTZ. au biashala za waTZ. binafsi ughaibuni, kwani ndiyo wanaelewa wateja wako wapi ambao wanaweza kuja bongo na unaongea navyo vipi kuwashawishi.Mfano:raia wa Ulaya, USA, Canada wanatofautina kimaitaji. Hata kwenye matangazo ya Tv. au matandao wangezisaidia balozi wajue wapi pa kutaget. Wazalendo ughaibuni wanajua mida ghani ni mizuri kwa likizo ya wageni kuja TZ. Vile vile si wanyama poli na Mlima kilimjaro ndio vivutio vya kila mtalii, bali wengine wanapenda kusaidia, elimu, michezo, dini n.k Kivutio kikubwa kutangazwa ingekuwa ukarimu wa watu TZ. Hii ni Ecomonics 101. Tanzania kuwatenga watu wake ni makosa na kunaonyesha jinsi serikali yetu isivyojua biashala. Mfano;mie mwenyewe mwaka huu nimeleta watu 50 bongo mwezi wa sita na saba, kwa sababu wakati huu shule huwa zimefunga kwa muda mrefu. na hapa kwa vile nilikuwa na watu kibao niliomba msaada ubalozi wa TZ.(Mh.naibu balozi akaniandikia e-mail kusema nimweleze nini naitaji lakini nilipomjibu aliniona kama msanii fulani-akufutalia tena).

    ReplyDelete
  8. La kushangaza sikumuona hata MZANZIBARI mmoja katika hiyo bodi inayoitwa ya Tanzania na mukiambiwa au kuitwa Watanganyika munakataa sana acheni kuongopea watu nyinyi mtabaki kuwa Watanganyika tu ndio asili yenu mkataa kwao mtumwa .GOD BLESS ZANZIBAR.

    ReplyDelete
  9. sasa jamani hata kuvaa kabendera kwenye hayo makoti yenu? maana mumepiga full western hata kakitengenge kwa mbali au scarf ya bazaaa!! Halafu mama hio saa ni yetu maana usije ukafikiri umepewa wewe binafsi, iwakilishe ofisini!!

    ReplyDelete
  10. ohh wazanzibar!!! ohh watanganyika!!! mibichwa mingine imejaa maji tu, TTB fanyeni kazi, suala la wazanzibar na watanganyika waachieni wanasiasa!! na hao mabichwa maji

    ReplyDelete
  11. Nimeandika makala ndefu ya kupost hapa kumbe ina limit, nitajibu kidogo tu hapa
    TTB ni ya Bara na Zanzibar iko Comission for Tourism Zanzibar ila walitakiwa kujiunga pamoja wanapotoka nje ya nchi wawe ni vyombo toka Tanzania ndio maana kwenye mambo ya TTB mara chache sana huoni Zanzibar, pia Zanzibar mambo ya utalii ni wa kwao ukienda Zanzibar kama wewe ni tour guide wa bara wanakukamata, hapo ndiko wanakosea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...