Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na India na Mhe. Debnath Shaw, Balozi wa India hapa nchini.
Balozi Mbelwa (wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Balozi Shaw (wa pili kutoka kushoto) wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Bw. Kunal Roy (kushoto), Afisa kutoka Ubalozi wa India hapa nchini na Bi. Redemptor Tibaigana (kulia), Afisa kutoka Idara ya Asia na Australasia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa.
Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimkaribisha Wizarani Bw. Hitokazu Okado, Makamu wa Rais wa  Kampuni ya Sumitomo ya Japan alipofika kwa mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji.
Balozi Kairuki (wa tatu kutoka kulia) akimsikiliza Bw.Okado  (wa pili kutoka kushoto) wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Bw. Tetsujiro Tani ( kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni  ya Sumitomo, Bi. Redemptor Tibaigana (Kulia), Afisa kutoka Idara ya Asia na Australasia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bw. Hasnein GulamHussein, Mkurugenzi wa Kampuni ya Sumitomo hapa nchini.
Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimkaribisha Wizarani Bw. Koji Nakamura, Mkurugenzi wa Kampuni ya NEC Afrika ya Japan inayojishughulisha na masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Bw. Nakamura alifika Wizarani kwa lengo la kuitambulisha teknolojia mpya  inayotumiwa na Kampuni yake ikiwa ni jitihada za kuimarisha sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini.
Bw. Nakamura akimuonyesha Balozi Kairuki moja ya teknolojia wanayoitumia katika masuala mbalimbali ya mawasiliano.
Balozi Kairuki akimsikiliza Bw. Nakamura alipokuwa akimuelezea masuala mbalimbali kuhusu teknolojia hiyo.
Bw. Ryoji Metsuoka (kushoto), mmoja wa Wataalam aliyefuatana na Bw. Nakamura (katikati) akifafanua jambo kwa Balozi Kairuki kuhusu Teknolojia hiyo ya kisasa ya mawasiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...