Mkutano Mkuu wa kufunga mwaka wa jumuiya ya Watanzania Rome, ambao ulikuwa ukisubiriwa na Watanzania wengi tokea mjini Roma na vitongoji vyake, ulifanyika kama ilivyopangwa saa kumi jioni jumamos ya tarehe 24 Novemba 2012. Mkutano ulifanyika kwenye mtaa wa Giovannni Lanza 122, mjini Roma karibia na Kituo cha Metro cha Termini.
Mkutano huu mkuu wa jumuiya ya Watanzania Roma, uliongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma, Mh. Leonce Uwandameno.
Kulingana na katiba ya jumuiya ya Watanzania Roma kipengele namba 6.1, mkutano huu ufanyika kila mwisho wa mwaka mwezi wa kumi na moja. Malengo ya mkutano kwa mwaka huu yalikuwa haya;
- Kujadili mwenendo wa jumuiya kwenye kipindi cha mwaka mzima wa 2012. Yaani mwenendo wa michango, ushirikiano baina ya jumuiya hii ya Roma na Jumuiya zingine za Kitanzania hapa Italy pamoja na Ubalozi wa Tanzania Italy. Wajumbe pia walijadili mafanikio yaliyoonekana kwenye mwaka wa 2012 na pia bila kusahau matatizo mbalimbali yaliyojitokeza na kuyatafuta suluhisho.
- Wanajumuiya pia walijadili juu ya Utambulisho wa huduma mpya ya BIMA kwa Watanzania waishio Diaspora. Hoja hii ilionekana kuwavutia waudhuliaji wengi ambapo kila mmoja alichangia mawazo tofauti ambapo uongozi wa jumuiya uliwaahidi wanajumbe kuwa utafikisha maoni yao kwa wahusika ili waweze kutoa maelezo zaidi juu ya hii BIMA.
- Kuwasihi wanajumuiya na watanzania wote kwa ujumla, juu ya umuhimu wa ushiriki wao kwenye kuchangia maoni kwenye mchakato mzima wa kufanikisha ukamilishaji wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
![]() |
| Mwenyekiti, Mh. Leonce Uwandameno akisikiliza hoja kutoka kwa mjumbe, pembeni yake ni Katibu, Andrew Chole Mhella. |
| Katibu, ndugu Andrew Chole Mhella akielezea mwenendo wa jumuiya kwa mwaka wa 2012. |
| Hii ni baadhi ya safu ya waudhuliaji. |
| Kwa nyuma ni Mwenyekiti Msaidizi Mh. Erasmus Pindu Luhoyo, kwa mbele kushoto ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe na Mikutano ndugu Bakari Hizza pamoja na Mjumbe Bi. Lucy M. upande wa kulia. |



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...