![]() |
MWENYEKITI WA MTAA HUO HABIBA MWAKITALU AMEMBEBA MTOTO ANETH TAYARI KWA KUMPELEKA HOSPITALI HUKU NYUMA AKIFUATIWA NA MWESHIMIWA DIWANI KATA YA MAJENGO SAMWELI |
![]() |
WANANCHI WENYE HASIRA KALI WALIMCHUKUA MAMA HUYO NA KUMPELEKA KITUO CHA POLISI |
Most read Swahili blog on earth
![]() |
MWENYEKITI WA MTAA HUO HABIBA MWAKITALU AMEMBEBA MTOTO ANETH TAYARI KWA KUMPELEKA HOSPITALI HUKU NYUMA AKIFUATIWA NA MWESHIMIWA DIWANI KATA YA MAJENGO SAMWELI |
![]() |
WANANCHI WENYE HASIRA KALI WALIMCHUKUA MAMA HUYO NA KUMPELEKA KITUO CHA POLISI |
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Huu ni unyama wa hali ya juu, yaani unafanya ukatili kama huu kwa mtoto ambaye hajui hata alitendalo masikini. ivi amekosa nini huyu mtoto mpaka umpe adhabu kali ya kula kinyesi na kumchoma moto? Hongera kwa majerani ambao waliamua kubomoa mlango ili kumuokoa mtoto nadhani ingekua mbaya zaidi kwa mtoto iwapo kusingekuwepo watu karibu. Nipo ulaya huu ni mwaka wa nane hakuna upendo kama huo ulioneshwa na hao majerani kwa kudiriki hata kuvunja mlango, huku jeerani humjui hakujui likitokea la kutokea ni la kwako peke yako. Hongera watanzania kwa kudumisha upendo na mshikamano.
ReplyDeletePole sana mtoto. Nimeumia sana, kama baba wa binti wa miaka mitatu. Ninakuombea upone na pengine kwa vile si rahisi urudi tena kwa huyu mama anayekutesa, basi Mungu akuweke kwenye mikono ya watu wanye upendo na kujali ili ukue vizuri kama watoto wengine. Nawashukuru saaana majirani kwa moyo wenu wa upendo na kujali. Kwa kweli watanzania pamoja na uswahili wetu, bado roho ya upendo tunayo. Mbarikiwe saaaaana!
ReplyDeletewewe au wa kwanza jiangalie wewe kama haujui majirani, navyojua mie wazungu ni wambea kupita hawawezi kaa kimya wakisikia kelele za watoto za kushtua kama hivi.
ReplyDeletemnapenda sema watu wana rohom
mbaya mbona hata Dar hapo majirani hawajuani hata kuzoeana kama zamani, imeanza wengi kila mtu na lake. hata watoto wanaojumuisha wazazi kujuana hawaonekani mitaana sana maeneo mengi wakicheza wote.
na nyie au wewe kuwa unasalimia sio wote roho mbaya as sie tunayo roho mbya hta ya kutesa wafanyakazi. sasa ukianza kuwaonyesha una utu utaona usipojiachia ukawa mwoga nao wanakupotezea wakizani haupendikujuana.
il ya kelele, ugomvi kusemewa na hao hao majirani ni namba moja. wanapiga polisi mambo mbele.
Wewe sema ilivyo usiseme ulipo.ulaya ulaya ndio nini Sasa Wewe mshamba wa ulaya? vipi Wewe
ReplyDeleteHaya, na huyo mama ni msomali?
ReplyDeletemi nazani huyu dada anamatatizo ya akili kwani mtoto wa miaka mitatu anajua nini niliposoma hii nilimwangalia mwanangu ambaye anamiaka mitatu, nikaona huyu akapimwe akili?mtoto bado ni mdogo sana huyo ajui hata kula mwenyewe, au ajazaaa heeeeeee.
ReplyDeleteHuyo mwanamke lazima atakuwa mchawi na ameshakula nyama ya mtu kama alivyosema nyerere, na afichwe asionekane tena duniani maana kizani chake kibaya hakitakiwa duniani.
ReplyDeletePOLE SANA MTOTO. MWENYEZI MUNGU NDIYE MUWEZA WA YOTE, AKUPONYE NA KUKUPA AFYA NJEMA.
ReplyDeleteYaani nimesikitika sana huyo mama mdogo mlivyomshika kwa kumbembeleza, angekuwa huku kwetu kwa kweli angejuta kuzaliwa. Maana akepata kipigo cha mbwa mwizi, walau na yeye auguze vidonda. Angefika polisi akiwa atamaniki, uso hasomeki.
Haya Sasa tungependa kujua kama na Huyo mama Ni msomali? Pole sana mtoto Mungu atakusaidia na Huyo mama lazima apelekwe mbele ya haki. Majirani hongera sana Kwa kazi mliyo fanya neibour watch Ni asili yetu wa bongo big credit to them majirani. Michuzi tafadhali to feedback mwisho wa kesi hiii
ReplyDeleteWEWE Mwanamke unyama uliomfanyia mtoto unastahili kunyang'anywa mtoto na wewe kufungwa Gerezani.
ReplyDeleteKama ulizaa na hutaki kumlea mtoto kwa kumdhalilisha na kumtesa kwa nini kama umeshindwa usimkabidhi mtoto kwa wengine alelewe?
Huyo mtoto sio wako pekee bali ni rasilimali ya nchi na wananchi kwa ujumla licha ya kuwa umemzaa wewe.
Unajuaje?, inawezekana unatutesea Raisi wetu wa baadae na sisi wa Tanzania hatuwezi kukubali kwa hilo!
Wabeba boxi utawajua kwa maandishi yao. Full frustration, full povu
ReplyDeleteHuu ukatili si wa kawaida. Huenda ana schizophrenia huyo dada. Anatakiwa apate huduma ya hospitali huyo. Mama na baba wa mtoto nao punguwani. Watamwachiaje mtoto wa miaka 3 mtu mwingine. Enyi wazazi, tukumbuke wajibu wetu kwa watoto.Tumewaleta wenyewe duniani ni jukumu letu sisi wenyewe midhali tuko wazima kuwalea na kuwalinda.
ReplyDeleteHongera kwenu majirani wa huyo katili, wameonyesha utu wa hali ya juu. Wamekuwa mfano wa kuigwa kwa jamii kwa kutovumilia hali hii. Ukweli hii social structure ya nyumbani ni katika mambo ambayo tunaya-miss tulioko ughaibuni.
huyo mama afanyiwe kama alivyo mfanyia mtoto ili aone uchungu kama huyo mtoto alivyo uona. huwezi kukaa na mtoto si umpeleke sehemu atakayopata msaada kweli mtoto wa miaka mitatu kweli???? anajua nini jamani laiti ningekuwa hapo sijui huyo mama ningemfanya nini naomba vyombo vya habari vifuatilie kwa kina na haki za binaadamu sijui wako wapi jamani.
ReplyDeleteKwa kweli nimeumia sana. Pole sana Aneth. Nafahamu machungu uliyoyapata. Kumbuka hata ukimwagiwa kikombe cha chai jinsi mtu unavyoumia sembuse kumwagiwa maji kwa mtindo huo?. Niseme kuwa kama mtu huwezi kumtunza mtoto wa mwenzio huna haja ya kujifanya unaweza kumtunza wakati roho yako ni mbaya au ina mtima nyongo. Akina baba mnaozaa nje ya ndoa na kukusanya watoto kuwapelekea wake zenu kwa mabavu hata kwa hiari kumbukeni haya ndio yanayowapata. Anaweza asimwagiwe maji lakini akapewa vijineno vidogo vidogo vikamfanya asiishi kwa raha na baba ukiarifiwa unakuja mbogo kwa huyo mtoto bila ya kufanya utafiti. Kumbukeni mtoto anayelelewa na mtu ambaye sio mama yake mzazi huwa hawana uhusiano wa karibu kwa kuwa kibaolojia hawana damu ya pamoja. Fungukeni jamani. Nina imani vyombo vya dola vitafanya kazi yake na sheria kuchukua mkondo wake ili adhabu kali itolewe kwa huyu binti ili kuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia ya aina hii.
ReplyDelete