Unapotaja majina ya wapiganaji wakongwe kisiwani Zanzibar hutokosa kutaja jina la Farouq Karim wa ITV ambaye toka asubuhi utasikia sauti yake ikipasha haya na yale karibu kila siku ya Mungu kwa miaka inakaribia 15 sasa. Faroq, ambaye jina lake la utani ni Zinadine Zidane 'Zizzu', amezaliwa na kukulia katika habari ambapo baba yake Mzee Karim (RIP) ndiye wakala mkuu wa magazeti Zanzibar toka enzi hizo katika duka lao la Masomo Bookshop, nyuma ya Markiti mitaa ya Shangani. Kazi hiyo ameirithi uzuri tu na anaendeleza Libeneke kama anavyoonekana katika taswira hizi
Hapa ni hesabu kwa kwenda mbele
Wadau wakipitia vichwa vya habari Masomo Bookshop, Zanzibar
Hawa watu wenye tabia ya kusomea magazeti ukutani au mezani wanaharibu biashara za wenzio. Unakuta mtu kasimama anasoma habari zote kisha anaondoka hanunui. Hivi ni tabia gani hii?
ReplyDeleteMdau, CA USA
marikiti nyuma shangani ndio vipi mbona unatuchanganya?
ReplyDelete