Pichani ni Sehemu ya Muonekano wa Baadhi ya Vikwangua Anga vinavyopendezesha jiji la Dar es Salaam kama vilivyonaswa mchana wa leo na Kamera ya Globu ya Jamii.Nani kasema Bongo mambo sio Tambarareeee???

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Du kama newyork amakweli bongo tambarare naamini baada ya mwaka mmoja nitarudi home na sitojilaumu. maana kama vikwangua anga si ndio kama hivi vya huku tu, aah maboksi basi wacha nirudi.

    ReplyDelete
  2. KWANI VIKWANGUA ANGA VINA MAHUSIANO GANI MAISHA YAKO YA KILA SIKU WEWE MDAU WA Sat Nov 10, 12:22:00 AM 2012 KAMA ULIVYOCHANGIA CHINI AU ULIENDA ULAYA KWA KUWA KUNA VIKWANGUA ANGA

    Du kama newyork amakweli bongo tambarare naamini baada ya mwaka mmoja nitarudi home na sitojilaumu. maana kama vikwangua anga si ndio kama hivi vya huku tu, aah maboksi basi wacha nirudi.

    Sat Nov 10, 12:22:00 AM 2012

    ReplyDelete
  3. Teh teh teh et bongo tambalale wakati kukinyesha mvua posta nzima inanuka yani haina tofauti na manzese tena afadhari ya manzese sikuizi kunabadilika mayb tandare wanako fungulia vyoo jamani kujenga majengo makubwa hayo yaendane nakuimarisha miundo mbinu ya maji taka yani majengo makubwa mitaro ya mkoroni hadi leo halafu hapo ndiyo katikati ya jiji ukizungumzia bongo hapo ndipo inapo anzia, ivi ikulu na ofisi ya waziri mkuu wanavumiliaje harufu ya feri jiji alifanyi kazi yake pamoja na wizara inayo husika.. maendeleo yaendane na miundo mbinu.

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza anonymous wa Sat Nov 10, 12:22:00 AM 2012

    ..KARIBU SANA NYUMBANI TANZANIA!

    Bongo tambarale kama unavyoona mita chache kama 200M-300M hivi pana Kile Kituo kikuu cha MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI DART-(DAR RAPID TRANSIT) ndio barabara imevunjwa Morogoro road na Samora kwa maandalizi huku Kampuni ya Kijerumani STRABARG GmbH ikiwa kazini kwa wiki ya pili sasa!

    Mpango ukikamilika baada ya hiyo miaka 3 nadhani Bongo itakuwa ni Tambarale na haina tofauti na majuu!!!

    Ahhh jamani mimi nafikiria kuirudisha Mamlaka ya Uhamiaji Pasipoti yangu ni vile sina mahitaji ya kuondoka hapa nyumbani Tanzania hivi karibuni !!!

    BONGO TAMBARALEEEEEEEEEEEEEEE!!!!

    ReplyDelete
  5. Ahsante sana Raisi Jakaya Kikwete na Timu yako kwa kazi nzuri!!!

    Na bado hapo kwa mauzo ya Gesi na Madini mengine, tunatarajia uwekezaji utashika kasi zaidi kipindi kinachofuata kwa Mitaji kuingiwa ktk Sekta ya Gesi, Mafuta na Madini nchini ndio tutashuhudia vikwangua anga zaidi.

    La muhimu Mikataba ipitiwe ili tuweze kuvuna mafao ya mali zetu kwa tija , huku rasilimali ikielekezwa kkuwekwa mikononi mwa Wananchi kwa njia ya MItaji na Masoko ya Hisa pamoja na Sera zinazoashiria kulinda maslaihi ya wananchi !!!

    Ili kuonegza kasi ya Ukuaji mambom haya ni muhimu:

    1-Mikataba ipitiwe upya na kutoa fursa zaidi kwa wananchi.

    2-Ziwekwe sera za kulinda maslahi yawafikie wananchi walio wengi dhidi ya uchu wa mabwenyewe wanaokuja kuwekeza kwa kigezo cha kutoa Mtaji, Uwezeshaji wa Kiuendeshaji na Teknolojia.

    3-Panahhitajika upanuzi hasa wa miundo mbinu usambazaji wa Gesi, Uhifadhi na Ufuaji wake 9viwanda vya mazoa ya gesi (Pertochemicals Industries).vitaleta
    -mapato makubwa kwa Pesa za Kigeni,
    -kuongeza uzalishaji mali nchini,
    -Kuhamisha Tekinolojia,
    -Kuitisha uwekezaji zaidi
    -kutoa ajira nchini.

    Wataalamu wamefanya tathimini ikanonekana kuwa kama Gesi itafikishwa ktk nchi hizi 5 za eneo la Afrika ya Mashariki (Tanzani, Kenya,Rwanda,Uganda na Burundi) inaeza kututoa kwa mapato ya mauzo yake licha ya Masoko ya nchi za nje ya eneo hili kama Asia, Ulaya na Marekani ambako ni mbali. Hivyo uwekezaji ktk Miundo mbinu ya Gesi ni muhimu sana kwa sasa hapa Tanzania.

    Hivyo kama tutaivuna Gesi kwa ufanisi ni wazi mapato hayo yanweza kuipendezesha zaidi tasiwra hii ya Tanznaia nzima (mikoa yote hadi Zanzibar) na sio Dar Es Salaam pekee kwa vikwangua anga.

    Mahala Mabilioni ya Dola yakiwekezwa ktk Mitaji ya Gesi ,Mafuta na Madini vikwangua anga vitakosekana?

    PAMOJA TUIJENGE TANZANIA!

    ReplyDelete
  6. Duhhhh!!!

    Bongo raha jamani weee !!!

    ReplyDelete
  7. Mimi nakaribia kuiweka Darini Pasipoti yangu!

    Kuna haja tena ya kwenda Majuu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...