Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi wa ‘Education for All Global Report’ ya mwaka 2012 inayoandaliwa na UNESCO kila mwaka, ambapo pamoja mambo mengi aliyoyazungumzia pia amesema tukiwa tumebakiwa na si zaidi ya miaka mitatu kufikia mwaka 2015, michakato ya kutimiza Malengo ya Maendeleo ya Millenia (MDGs) na Malengo ya ‘Elimu Kwa Wote’ (EFA) lazima irekebishwe.
Ameongeza kuwa japo Tanzania inakaribia kutimiza lengo namba 2 la MDGs la ‘Elimu ya Msingi kwa Wote na lengo la Tatu la Usawa wa Kijinsia lakini bado ziko changamoto, akitolea mfano katika elimu na kusema msisitizo umeelekezwa katika kuongezwa kwa idadi ya watoto wanaojiunga shule lakini kimsingi kinachotakiwa ni kuweka mkazo kwenye kiwango cha elimu kinachotolewa.
Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen akiwasilisha matokeo ya ripoti ya 10 ya ya mwaka 2012 ya ‘Education for All Global leo jijini Dar es Salaam inayoitwa “Putting Education to Work” na kufafanua kuwa takriban vijana milioni 2 nchini Tanzania hawajamaliza elimu ya msingi na hawana maarifa ya kuwapatia kazi itakayowapatia kipato cha kujikimu kimaisha.
Amesema matokeo ya ripoti hiyo yanaonyesha kuwa juhudi za haraka zinahitajika ili kuwekeza katika kuwapatia vijana elimu haswa wenye miaka kati ya 15 hadi 24 Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
KUINUA MWAMKO WA ELIMU KWA VIJANA NCHINI:
ReplyDeleteDUNIANI HAPA NCHI KADHA ZIMEREKEBISHA TARATIBU ZA KUTOA ELIMU YA JUU ILI KUWEZA KUWAFIKIA WENGI KWA KUZINGATIA HAYA HAPA CHINI:
1.KUWALENGA HASA WALE WALIO KTK MAZINGIRA YALIYOFUNGIKA KAMA WALIO SEHEMU ZA KAZI,
2.KUPUNGUZA MASHARITI YA SIFA ZA KUJIUNGA NA ELIMU YA JUU, KAMA KUTOFAUTISHA KATI YA MTAFUTA ELIMU KWA SOKO LA AJIRA, ANAYETAKA ELIMU YA KUJIAJIRI AMA KUENDELEA NA ELIMU ZAIDI.
3.KUTOA RUZUKU KWA WANAOTAKA MASOMO AMA KUPUNGUZA GHARAMA ZA ELIMU AMA KUTOA MIKOPO ZAIDI.
NAFIKIRI KAMA VYUO VIKUU VITAZINGATIA HAYO MATATU KAMA KUELTA CAMPUS ZAO KATI KATI YA MIJI KWA WAFANYA KAZI NA VIJANA NA MASUALA YA MAMLAKA KUTOA UWEZESHAJI KWA WANAOYAKA MASOMO NAFIKIRI ELIMU ITANAPANDA NCHINI NA KUFIKIA HAYO MALENGO YA MILENIA MDG's
Ari ya kusoma kwa wengi wa wa Tanzania imeanguka saaana.
ReplyDeleteAngalia hata Makala hii imekosa hata mchangiaji mmoja tokea iwekwe jana.
Ukitaka kuona kuwa ari ya masomo imeanguka sana kwa jamii yetu ya Tanzania utaona m Tanzania anasoma endapo yanatokea moja ya haya hapa:
1-Kazini kwake pana mpango wa kupunguza wafanyakazi anasoma ili aweze kubakishwa kazini kwa Elimu ya ziada tena iliyo ktk mwelekeo wa kazi aliyoipata.
2-Kazini kwake pana Waajiriwa wageni na hasa waliotoka Kuhitimu karibuni hivyo mwenyeji anasoma ili aweze kupanda Cheo na kuwa juu.
3-Kazini kwake hasa ktk Idara za Serikali na Majeshi pana Majukumu ambayo anataka kuyakwepa hivyo njia rahisi ni kuingia ktk masomo ili asipangwe ktk kazi hizo.
Mara zooote anayesoma anaonekana anatokea Sayari ingine.
Si mnaona hata Maktaba Kuu vitabu vimejaa mavumbi kibao ?