MARA kwa mara jamii imekuwa ikisikia Wanajeshi wakiwapiga Askari wa Usalama barabarani hasa Jijini Dar es Salaam Trafiki wa Moshi huenda wamechoshwa na unyanyasaji huo kwa walinzi hawa wa amani na wasimamizi wa sheria ambapo huko Mkoani Kilimanjaro, Askari wa kikosi cha usalama barabarani mjini Moshi ambao majina yao hayakufahamika walimpiga askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kituo kikuu cha mabasi hivi karibuni,baada ya kutokea kutoelewana,mwanajeshi huyo alikuwa akimtetea dereva wa Hiace aliyeshikwa na trafiki hao kwa kufanya kosa la kiusalama barabarani.jambo hili halikuwa la kawaida kuonekana machoni mwa watu lakini hivi ndivyo ilivyokuwa.Picha na Nakajumo James wa FK Blog.
Home
Unlabelled
Mwanajeshi Mkoani Kilimanjaro achezea kipigo toka kwa Askari wa Usalama barabarani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




WATARUDI USIKU HAO KULIPIZA KISASI... WAULIZENI WANANCHI WA KIGAMBONI MIAKA 10 ILIYOPITA.
ReplyDeleteHivi siyo vitu vya kushabikia, kwasababu hawa ni walinzi wetu, na hivyo hawapaswi kuchukiana kwa vile ni wamoja.
ReplyDeleteSijui kwanini mambo haya yanatokea au mpaka wapate semina na wenyewe kama hao waendesha pikipiki?
Halafu mnadhani hiyo vita imeisha,ninavyo wafahamu mimi wanajeshi hapo anaenda kuchukua wenzake mtasikia kipigo kitakacho washukia hao traffic police tena watakuja na Machine gun,tayari kwa vita, mjue kwamba hao wamefundishwa kuua,Proffesional killers kama hamjui.
ReplyDeleteHao [Transport/traffic]polisi sheria za nchi wanazijua sawsawa wamepigana hadharani hivyo wanatakiwa kufuzwa kazi, na huyo army officer afanyiwe uchunguzi kama amevunja sheria,jeshi limuachishe kazi na ashitakiwe mahakama ya kawaida,hawa wote wanaonyesha mfano gani kwa raia wa kawaida
ReplyDeleteTanzania inaelekea pabaya kama hawa wanausalama wanafanya vitendo kama hivi tena mbele ya raia inasikitisha sana, halafu watu wanakwambia bongo tambarale, heheheeeee....haya tutaona yataishia wapi.
ReplyDeletepolisi hawa wanaonekana kutojua sheria ya kijeshi,upaswi kumdharirisha mtu yeyote mwenye yunifomu na ikiwa ya kijeshi ndio kabisa upaswi kumgusa,kama ningekuwa CO wa huyo askari kijana hapo ni kurudisha heshima ya jeshi hao askari polisi aka (raia wakakamavu)wanatakiwa kikosini within 2 hrs kwa njia yoyote ile wapatikane na platoon moja tu inatakiwa kukamata hao.wakifika kikosini watakutana na MP wa zamu ambaye atawajulisha vazi la jeshi linaheshima gani hapa tanzania na dunia nzima.
ReplyDeleteBy Nyamongo mmoja
hahaaaaa ,, watu weusi mhhhhhh
ReplyDeleteHuyu mwanajeshi anaonekana ni mgeni na mpya maana yule mzoefu uwezi kamatwa hata siku moja na askari polisi hivi.IGP chukua taadhari kwa vijana wako wanatafuta kasheshe,CDF ruhusu vijana warudishe heshima ya jeshi.
ReplyDeleteWanajeshi wanajifanyaga wao wako juu ya sheria,baada ya kumdhibiti hivyo anatakiwa afikishwe mbele ya sheria. Wanadekezwa sana hao na kujiona waoni bora zaidi kuliko wote.
ReplyDeleteVery stupid .. the are no rule of laws. Police and Army should not harass people. If someone breaks the law charge him/her. This is so uncivilized. Police are supposed to use force only if someone resists an arrest.
ReplyDeletePOLICE IN KILIMANJARO ARE SO CORRUPTED. I witnessed this on my very eye. Wake up Tanzania!
Mdau Canada!
VITA NI VITA MURAA
ReplyDeletePolisi wamekosa kutumia utaalam wao kwenye hili, a man in uniform anatakiwa apewe heshima yake. Polisi walitakiwa kuchukua maelezo ya huyo mwanajeshi au namba yake na kuripoti kituoni kwa hatua zaidi lakini si hicho walichokifanya.
ReplyDeleteUTOVU WA NIDHAMU NI KITU KIBAYA.
ReplyDeleteINAELEKEA HUYU MWANAJESHI YUKO RIGHT, KWA NINI HAO WALIOVAA NGUO NYEUPE WASIFUATE SHERIA.
ReplyDeleteNAJIVUNIA JESHI SHUPAVU LA WANANCHI WA TZ.
Ukitumia neno 'uncivilized' majamaa wanamind lakini hawa wote hawa akili zao ziko ************! Laini there are ni law enforcements in Tanzania. Hili ni tatizo sugu!
ReplyDeletePolisi wanapiga raia! kimya!
ReplyDeletePolisi wanakula rushwa! kimya!
Polisi wanabambikiza kesi! kimya!
nyani wamemaliza miti....
kesho utasikia waziri kachezea kipigo cha polisi.....wallahi tena!
wanajeshi waliwapiga polisi ubungo sikuona maoni ya kuwatetea polisi humu, je wao hawakuwa wamevaa uniform? huyo mwanajeshi hakutakiwa kuingilia kazi isiyomuhusu, mwanajeshi asiyejua mipaka yake huyo sio mwanajeshi hata kama ana uniform huyo ni muhuni ndani ya jeshi anatakiwa kuondolewa haraka sana, na ninyi polisi jirekebisheni, wanajeshi wamewapiga ubungo hakuna mtu amekuwa upande wenu, ninyi mmemdhibiti tu huyo mwanajeshi watu wanawalaumu, ooh mmempiga! kwasababu mna maovu mengi.
ReplyDeleteSasa raia tufanyeje? Haya ni moja tu ya matokeo ya udhaifu mkubwa uliopo kwenye majeshi yetu. Ajira za kupeana kwa kujuana na kupendeleana bila weredi wa mtu.
ReplyDelete