MARA kwa mara jamii imekuwa ikisikia Wanajeshi wakiwapiga Askari wa Usalama barabarani hasa Jijini Dar es Salaam Trafiki wa Moshi  huenda wamechoshwa na unyanyasaji huo kwa walinzi hawa wa amani na wasimamizi wa sheria ambapo huko Mkoani Kilimanjaro, Askari wa kikosi cha usalama barabarani mjini Moshi ambao majina yao hayakufahamika walimpiga askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kituo kikuu cha mabasi hivi karibuni,baada ya kutokea kutoelewana,mwanajeshi huyo alikuwa akimtetea dereva wa Hiace aliyeshikwa na trafiki hao kwa kufanya kosa la kiusalama barabarani.jambo hili halikuwa la kawaida kuonekana machoni mwa watu lakini hivi ndivyo ilivyokuwa.Picha na Nakajumo James wa FK Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. WATARUDI USIKU HAO KULIPIZA KISASI... WAULIZENI WANANCHI WA KIGAMBONI MIAKA 10 ILIYOPITA.

    ReplyDelete
  2. Hivi siyo vitu vya kushabikia, kwasababu hawa ni walinzi wetu, na hivyo hawapaswi kuchukiana kwa vile ni wamoja.
    Sijui kwanini mambo haya yanatokea au mpaka wapate semina na wenyewe kama hao waendesha pikipiki?

    ReplyDelete
  3. Halafu mnadhani hiyo vita imeisha,ninavyo wafahamu mimi wanajeshi hapo anaenda kuchukua wenzake mtasikia kipigo kitakacho washukia hao traffic police tena watakuja na Machine gun,tayari kwa vita, mjue kwamba hao wamefundishwa kuua,Proffesional killers kama hamjui.

    ReplyDelete
  4. Hao [Transport/traffic]polisi sheria za nchi wanazijua sawsawa wamepigana hadharani hivyo wanatakiwa kufuzwa kazi, na huyo army officer afanyiwe uchunguzi kama amevunja sheria,jeshi limuachishe kazi na ashitakiwe mahakama ya kawaida,hawa wote wanaonyesha mfano gani kwa raia wa kawaida

    ReplyDelete
  5. Tanzania inaelekea pabaya kama hawa wanausalama wanafanya vitendo kama hivi tena mbele ya raia inasikitisha sana, halafu watu wanakwambia bongo tambarale, heheheeeee....haya tutaona yataishia wapi.

    ReplyDelete
  6. polisi hawa wanaonekana kutojua sheria ya kijeshi,upaswi kumdharirisha mtu yeyote mwenye yunifomu na ikiwa ya kijeshi ndio kabisa upaswi kumgusa,kama ningekuwa CO wa huyo askari kijana hapo ni kurudisha heshima ya jeshi hao askari polisi aka (raia wakakamavu)wanatakiwa kikosini within 2 hrs kwa njia yoyote ile wapatikane na platoon moja tu inatakiwa kukamata hao.wakifika kikosini watakutana na MP wa zamu ambaye atawajulisha vazi la jeshi linaheshima gani hapa tanzania na dunia nzima.

    By Nyamongo mmoja

    ReplyDelete
  7. hahaaaaa ,, watu weusi mhhhhhh

    ReplyDelete
  8. Huyu mwanajeshi anaonekana ni mgeni na mpya maana yule mzoefu uwezi kamatwa hata siku moja na askari polisi hivi.IGP chukua taadhari kwa vijana wako wanatafuta kasheshe,CDF ruhusu vijana warudishe heshima ya jeshi.

    ReplyDelete
  9. Wanajeshi wanajifanyaga wao wako juu ya sheria,baada ya kumdhibiti hivyo anatakiwa afikishwe mbele ya sheria. Wanadekezwa sana hao na kujiona waoni bora zaidi kuliko wote.

    ReplyDelete
  10. Very stupid .. the are no rule of laws. Police and Army should not harass people. If someone breaks the law charge him/her. This is so uncivilized. Police are supposed to use force only if someone resists an arrest.
    POLICE IN KILIMANJARO ARE SO CORRUPTED. I witnessed this on my very eye. Wake up Tanzania!

    Mdau Canada!

    ReplyDelete
  11. VITA NI VITA MURAA

    ReplyDelete
  12. Polisi wamekosa kutumia utaalam wao kwenye hili, a man in uniform anatakiwa apewe heshima yake. Polisi walitakiwa kuchukua maelezo ya huyo mwanajeshi au namba yake na kuripoti kituoni kwa hatua zaidi lakini si hicho walichokifanya.

    ReplyDelete
  13. UTOVU WA NIDHAMU NI KITU KIBAYA.

    ReplyDelete
  14. INAELEKEA HUYU MWANAJESHI YUKO RIGHT, KWA NINI HAO WALIOVAA NGUO NYEUPE WASIFUATE SHERIA.

    NAJIVUNIA JESHI SHUPAVU LA WANANCHI WA TZ.

    ReplyDelete
  15. Ukitumia neno 'uncivilized' majamaa wanamind lakini hawa wote hawa akili zao ziko ************! Laini there are ni law enforcements in Tanzania. Hili ni tatizo sugu!

    ReplyDelete
  16. Polisi wanapiga raia! kimya!
    Polisi wanakula rushwa! kimya!
    Polisi wanabambikiza kesi! kimya!

    nyani wamemaliza miti....
    kesho utasikia waziri kachezea kipigo cha polisi.....wallahi tena!

    ReplyDelete
  17. wanajeshi waliwapiga polisi ubungo sikuona maoni ya kuwatetea polisi humu, je wao hawakuwa wamevaa uniform? huyo mwanajeshi hakutakiwa kuingilia kazi isiyomuhusu, mwanajeshi asiyejua mipaka yake huyo sio mwanajeshi hata kama ana uniform huyo ni muhuni ndani ya jeshi anatakiwa kuondolewa haraka sana, na ninyi polisi jirekebisheni, wanajeshi wamewapiga ubungo hakuna mtu amekuwa upande wenu, ninyi mmemdhibiti tu huyo mwanajeshi watu wanawalaumu, ooh mmempiga! kwasababu mna maovu mengi.

    ReplyDelete
  18. Sasa raia tufanyeje? Haya ni moja tu ya matokeo ya udhaifu mkubwa uliopo kwenye majeshi yetu. Ajira za kupeana kwa kujuana na kupendeleana bila weredi wa mtu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...