Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Israel Kamuzora akitoa hotuba yake katika hafla ya kutimiza miaka 45 ya tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya Bima ya Ndege na Uzinduzi wa Nembo Mpya ya Kampuni hiyo,iliyofanyika usiku wa leo kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege,Sebastian Ndege (kulia) akizungumza machache juu ya Kampuni yake hiyo kabla ya kugonganisha Glass na Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Israel Kamuzora (kushoto) ikiwa ni ishara ya pongezi kwa Kampuni hiyo kuadhimisha Miaka 45 tangu kuanzishwa kwake.Hafla hii imefanyika usiku wa leo kwenye hoteli ya Serena,Jijini Dar es Salaam.
Keki ya Kuadhimisha Miaka 45 ya Kampuni ya Bima ya Ndege (Ndege Insurance) ikikatwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege (Ndege Insurance),Sebastian Ndege (kulia) akimuonyesha Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Israel Kamuzora (pili kulia) nembo mpya ya Kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wake rasmi ulioenda sambamba na kuadhimishwa kwa Miaka 45 ya tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo.
Mfanyakazi aliekaa kwa kipindi kirefu kwenye Kampuni ya Bima ya Ndege,Bi. Eutropia Benedict akikabidhiwa tuzo na mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni hiyo,Justine Ndege.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege,Sebastian Ndege (kushoto) akimkabidhi Tuzo ya heshima Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Israel Kamuzora (kulia) kwa mchango mkubwa alioutoa kwenye Kampuni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Miaka 45?? Walikuwa wanatoa bima sehemu nyingine au? Manake tangu soko huria la bima liingie nchini ni si chini ya miaka 12 iliyopita.

    ReplyDelete
  2. Mkuu naona kama hujakuwa na habari au taarifa zilizo sawa, Ndege insurance brokers ilianza kama insurance agency 1967 na ilianzishwa na mzee Casmir Bigacho Ndege baba wa Dr Sebastian Ndege wakiwa mawakala wa bima wa NIC- National Insurance Corporation of Tanzania, soko la bima kuwa huria lilikuwa kwa makampuni ya bima siyo mawakala.

    ReplyDelete
  3. Hongera Ndege Insurance kwa miaka 45 ya huduma!

    Mdau wa kwanza usishangae miaka 45 ya huduma, ni kuwa maisha hayakuanza tokea ulipozaliwa wewe, ukumbuke Soko Huria la Bima lilikuwepo tokea miaka hiyo huko nyuma ila lilidorora kubadilika kulingana na mielekeo ya Kiitikadi tuliyofuata nchini baada ya Uhuru.

    ReplyDelete
  4. Hongera saaana Ndege Insurance Brokers!!!

    Hizi ndio Kampuni zinazofaa kuwa kigezo chema cha 'Corporate Gorvenance' yaani Uendeshaji Unaokubalika wa Makampuni.

    Tumeshuhudia Fisadi ya kiuendeshaji hapa nchini mfano Kampuni moja kuanza baada ya miaka 10 imebadili majina na Wamiliki mara 3 au 4 hivi.

    Sasa kama Ndege Insurance Brokers ingekuwa sio kigezo chema nadhani kwa miaka hiyo 45 ya utendaji wake ikiwa na jinalille lile ingekuwa imebadili Wamiliki au Majina mara 15 au 20 hivi huenda sasa hivi isingekuwa ajabu kukuta ikiitwa ''KUNGURU INSURANCE BROKERS'' !!!

    ReplyDelete
  5. huyo mdau wa kwanza amelala usingizi,Ndege ni Broker .na wenzako hapo juu wamekujibu vema kabisa.
    inabidi na sisiwa tz tujue kuwa tukiwa na good foundation kwenye bness yeyote tunaweza kuwaachia watoto wetu uridhi mzuri,check jinsi watoto wa mzee ndege wanavochapa kazi wakati muanzilishi alikuwa babayao na alishafariki siku nyingii, watoto wanaienzi biashara kama kawa, yaani wamekuwa kama wahindi baba akianzisha kitu hakifi kizembezembe.
    Ila hii ngozi yetu hii mojority tunagawana chetu mapema na kila mtu kufa na chake... Wapi Joshua Ndege Crdb azikiwee?!!!Gud.

    ReplyDelete
  6. mdau wa Thu Nov 22, 10:01:00 AM 2012 umenifurahisha sana eti KUNGURU BROKERS...... NIMECHEKA KWA KWELI...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...