LIGI Kuu ya Tanzania bara mzunguko wa pili ipo kwenye hati hati ya kutofanyika baada ya
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuzifungia akanti za Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) kutokana na TFF kudaiwa zaidi ya milioni 100 na TRA.
Hatua hiyo ya TRA ya kuzifungia akaunti hizo za TFF, imekuja baada ya TFF kukiuka
taratibu za kuwakatia kodi makocha wa kigeni wanaozifundisha timu za Taifa tangu
kipindi cha Mbrazil Marcio Maximo.
Akizungumza kwenye ukumbi wa hostel za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kaimu
katibu mkuu wa shirikisho hilo ambaye pia ni mkurugenzi wa ufundi, Sunday Kayuni
alisema kutokana na hatua ya TRA kuzifungia akaunti hizo huenda Ligi Kuu mzunguko
wa pili isifanyike kutokana moja ya akaunti hizo kuwa na zaidi ya Sh.350m za klabu
ambazo zimetoka katika kampuni ya Vodacom ambayo ndiyo mdhamini wa ligi hiyo.
"Akaunti zetu zote zimesimamishwa na TRA kwa kile kilichodaiwa kuwa hatujalipa zaidi
ya sh 100 milioni za kodi za mishahara ya makocha wote waliowahi kuzifundisha timu za
taifa kuanzia kipindi cha Maximo hadi Sasa."alisema Kayuni
".
Kufatia hali hiyo kunauwezekano mkubwa wa Ligi Kuu mzunguko wa pili kutofanyika
kwa sababu moja ya akaunti hizo ilikuwa na zaidi ya sh 350 za klabu kutoka Kampuni ya
Vodacam wadhamini wakuu
"Wote tunafahamu kuwa hali halisi ya klabu zetu kiuchumi hivyo kufungiwa kwa akaunti
hizo kutaathiri moja kwa moja mchakato mzima wa ligi kwani timu nyingi zinategemea
fedha hizo kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na maandalizi ya ligi" alisema
Alisema.
TRA kufungia akaunti za TFF, imekiuka taratibu za kodi kwani shrikisho hilo
halipaswi kulipa kodi hiyo kwa sababu siyo linalolipa mishahara ya makocha hao.
Alisema Kodi hiyo ilipaswa kulipwa na Serikari ambayo ndiyo inayolipa mishahra ya
makocha hao na siyo TFF.
"Hakika hatujatendewa haki na huu ni uonevu, hatahivyo pia tumejaribu kufuatilia lakini
tumekuwa tukipigwa danadana....."
Pia tunasikitika Serikali kupitia Wizara ya Habari
Utamaduni na Michezo haionyeshi ushirikiano juu ya jambo hili ambalo linatufanya tuone
kuwa kuna kitu hapo katikati," alisema Kayuni ambaye alikuwa samabamba na
Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Said Mohamed pamoja na Mtendaji Silas Mwakibinga.
Katika hatua nyingi Kayuni alisema kuwa wapo kwenye mchakao wa kuunda kamati
maalum itakayohusisha TFF pamoja na wawakilishi wa klabu ili iweze kukutana na TRA
kwa mara nyingine tena kuangalia uwezekano wa kutatua tatizo hilo.
Hata hivyo Kayuni alisisitiza kuwa TFF haitalipa kodi hizo na haina fedha za kulipa
sababu siyo inayotakiwa kufanya hivyo kwa mijibu wa sheria ya kodi sababu siyo inayolipa
mishahara ya makocha hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...