Ndege
iliyokuwa imembeba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Mizengo Kayanza Pinda ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Mpanda
mapema hii leo. Waziri Mkuu atakuwa Wilayani Mpanda kwa shughuli kuu
mbili ambayo moja ni kikao cha tathmini ya kongamano la uwekezaji
lililofanyika wilayani hapa Oktoba mwaka jana pamoja na uzinduzi wa Mkoa
mpya wa Katavi ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mhe. Makamu wa Rais Dkt.
Mohammed Gharib Billal na kilele itakuwa siku ya jumapili tarehe
25/11/2012.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda
akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Col. Mst. Issa Machibya mara
baada ya kuwaisili katika uwanja wa ndege wa Mjini Mpanda mapema hivi
leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda
aikipokea maelezo kuhusu uwekezaji kutoka kwa Muwezeshaji katika banda
la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Bwana Misasi Nyanda Marco ambaye pia ni
Afisa katika dawati la uwekezaji.
Katibu
Tawala Mkoa wa Katavi Mhandisi Emmanuel Kalobelo akifurahia jambo na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mhe. Marry
Nagu wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda leo katika uwanja wa ndege wa mjini
Mpanda.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mhe. Marry Nagu mapema leo asubuhi kwenye mapokezi ya Mhe. Waziri Mkuu katika uwanja wa ndege wa Wilayani Mpanda.Picha na Hamza Temba,Katavi.
Ankal swali la kizushi kwako la kukupatia usingizi...Siku hizi naona kama kuna Camera zikipiga ndege kama hiyo inayotembea na pangaboya zinazunguka,picha inatoka kama pangaboya zilivyokuwa yaani unaona kwamba pangaboya zilikuwa zinazunguka(Ni kweli zipo au ni photo editor? au setting ya Camera?),na kuna Camera kama hii iliyotumika hapa Pangaboya zinaonekana zimetulia.Ndiyo,kwenye fizikia tuliambiwa pangaboya zinatakiwa zionekane zimetulia,mambo ya mwendo wa mwanga wa Kamera n.k.Lakini naona kama siku hizi hiyo 'law' inapitwa na wakati.Karibu Ankal
ReplyDeleteDavid V