Meneja wa Tanesco mkoa wa Temeke Eng. Richard Malamia akiwa na ofisa Mipango wake Bi. Cecilia Msangi wakiangalia nguzo ambayo haina sifa ya kusambazia umeme ambayo inasadikiwa imewekwa na vishoka katika maeneo ya Mbagala, Chamazi kwa Musoma jijini Dar es salaam leo. Eng. Malamia alifanya ukaguzi wa kustukiza  katika maeneo hayo akishirikiana na watalamu wake baada ya kupokea  malalamiko ya kuwepo kwa upungufu wa umeme katika maeneo hayo. Baada ya kufanya ukaguzi  alibaini kuwepo na watu waliojiunganishia umeme visivyo halali kupitia nguzo hiyo. Chini akiongea na baadhi ya wakaazi wa eneo hilo akiwa na wasaidizi wake. Picha na Chris Mfinanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani ifike mahali tuwajue hao vishoka ni akina nani kama si kikulacho!!?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...