Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema (pichani),
amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi.
Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa
Polisi mkoa wa Pwani SACP Ernest Mangu anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mwanza kuziba pengo la marehemu ACP Liberatus Barlow, ACP David Misime aliyekuwa
kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma
kuchukua nafasi ya SACP Zelothe Steven anayestaafu. Vilevile, aliyekuwa kamanda
wa Polisi Viwanja vya Ndege ACP Ulrich Matei anakwenda kuwa kamanda wa Polisi
mkoa wa Pwani.
Aidha, wengine ni kutoka Makao Makuu ya Polisi na
Makao Makuu Idara ya Upelelezi ambapo ACP Engelbert Kiondo kutoka makao makuu
Idara ya Upelelezi anakwenda kuwa kamanda
wa Polisi mkoa wa Temeke, ACP Rashid Seif kutoka Makao Makuu ya Polisi Kwenda
kuwa Kamanda wa kikosi cha Tazara, ACP Deusdedit Kato kutoka Makao Makuu ya
Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, ACP Shaban Hiki kutoka
Kamanda wa Kikosi cha Ufundi kwenda Makao Makuu ya Polisi na ACP Lucas Mkondya
kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Kikosi cha Ufundi.
Mabadiliko hayo pia yamehusisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu
wa kikosi cha Usalama Barabarani ACP Johansen Kahatano anayekwenda kusimamia Mradi wa SMARTER Traffic ambapo nafasi yake
itachukuliwa na aliyekuwa RTO mkoa wa Pwani ACP Swalehe Mbaga.
Uhamisho huo pia
umewahusisha baadhi ya Wakuu wa Operesheni wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi vya
Kutuliza Ghasia vya Mikoa, Wakuu wa Polisi wa Wilaya na Wakuu wa Upelelezi wa
Wilaya.
Uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni,
taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera
Senso-ASP
Msemaji wa
Jeshi la Polisi (T).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...