Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila mjini Kampala Uganda leo baada ya kumalizika kwa mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa makuu.Mkutano huo ulijadili hali ya usalama ya Mashariki ya DRC eneo ambalo limetekwa na waasi wa kikundi cha M23.Baadaya Rais Kikwete na ujumbe wake walirejea jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere muda mfupi baada ya kuwasili kutokea Kampala,Uganda ambapo alihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa makuu. (picha na Freddy Maro)

Raisi Kabila anahitaji msaada wetu kupambana na hao waasi ambao wanasaidiwa na Rwanda na Uganda. Vita hapo ni hayo madini yabayotumika kwenye smart phones, lakini pia na utajiri mzima wa Congo. Congo ni majirani wetu na tuna mpka mrefu na wao. Security ya Congo pia itahakikisha usalama wetu. Hii ilikuwa sifa yetu miaka ya nyuma tulipigania haki na ukombozi wa nchi nyingine pale tulipoweza. Nimezungumza na WaCongo wanasema ni raisi mzuri waliyewahi kumpata. Ni kijana wetu mpaka wako wachache wanaofikiria ni mtanzania sababu anaongea kiswahili na lugha na tamaduni za kwao hafahamu hivyo. Hivyo nguzo yake kubwa ni Bongo.
ReplyDelete