Leo jiji la Dar es salaam limegubikwa na wingu tokea asubuhi, lakini hii haimzuii Ankal kutukumbusha enzi za Osibisa  na wimbo wao wa chacha wa Sunshine Day. Osibisa, iliyoundwa mwaka 1969 jijini London na wana Diaspora wanne toka Ghana, na watatu kutoka Carribean, ilitamba sana enzi hizo za miaka ya 70

Wengi walijifunza kucheza  chacha kwa ngoma hii  wanamuziki waanzilishi wakiwa  Teddy Osei (saxophone,flute, na kuimba), Mac Tontoh (trumpet na kuimba viitikio), Sol Amarfio (drums na kuimba), wote wakiwa wametoka Ghana, Loughty Lassisi Amao (congas, percussion, na midomo ya bata), ftoka Nigeria, Robert Bailey (keyboards), toka  Trinidad, Spartacus R (bass), toka  Grenada, na  Wendell Richardson (gitaa la kwanza na kuimba)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ankal umetukumbusha mbaaaali!!!
    1975/1976 Secondary za Dar wakati tunakwenda kulima RUVU sekondari, Tunakaa Kibaha, Na kuna bwana mdogo mmoja alikuwa anacheza chacha sana kutoka forodhani. Sijui kama kuna jamaa wanakumbuka enzi hizo.

    ReplyDelete
  2. Ewe Bwaaana usinijuuee nenda kwanza ka... (naogopa kumalizia) haha umenikumbusha mbaali Michu

    ReplyDelete
  3. Enzi zile John Kitime alikua bado kijijini na kuja jijini Dar ilikua issue yaani kwa John Kitime alikua akisikia habari za jiji la Dar...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...