Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi barabara ya Issuna-Manyoni akiwa na viongozi wa serikali na wa TANROADS pamoja na wabunge wa mkoa wa Singida.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua ujenzi wa Barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya mkoani Singida leo. Pembeni yake kulia ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na viongozi wa serikali na wa kampuni ya ujenzi baada ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya mkoani Singida leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya mkoani Singida leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua ujenzi wa Barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya mkoani Singida leo.
Sehemu ya barabara mpya karibu na mji wa Manyoni iliyozinduliwa leo na Rais Kikwete.
Sehemu ya barabara mpya iliyozinduliwa na Rais Kikwete karibu na mji wa Katesh mkoani Manyara.
Sehemu ya barabara mpya iliyozinduliwa na Rais Kikwete mkoani Manyara.
PICHA NA IKULU
hapa mkulu anahitaji sifa zake kazi imefanyika.
ReplyDeleteNinapenda kuipongeza sana serikali ya Tanzania kwa juhudi zinazofanyika kuwaletea mabadiliko wananchi. Mungu ambariki Rais wetu Jakaya Kikwete na wasaidizi wake wote.
ReplyDeleteJamani mimi siipendi sana CCM lakini kwa hili la ujenzi wa barabara JK anastahili pongezi, tena nyingi tu. Hakuna rais yeyote wa Tanzania aliyefanya kazi kubwa kuendeleza miundombinu ya usafiri kama Kikwete, ambaye amekuwepo madarakani kwa miaka saba tu. Huu ni ukweli usiopingika. Kwa sasa Tanzania ndiyo nchi yenye mtandano wa barabara kuu (trunk road network) bora zaidi Afrika Mashariki na Kati.
ReplyDeleteWangetazama na namna ya kupunguza foleni kwenye miji mikubwa.
ReplyDelete