Mheshimiwa Ndugulile akisikiliza swali toka kwa
Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango
 Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Faustine Ndungulile amesema kamwe hajawahi kupinga ujenzi wa mji wa Kigamboni bali alitaka serikali imhakikishie kuwa wananchi wanashirikishwa katika hatua ya maamuzi  juu ya mradi wao. 

Mheshimiwa Ndugulile ameyasema hayo wakati akijibu swali kuhusu msimamo wake juu ya mradi huo katika kipindi cha Makutano, Magic FM.  Mradi huo ambao sasa ni miaka minne tangu uanze kuongelewa umezua mjadala mkubwa kwa wakazi wa Kigamboni, huku Mhe Ndugulile akitolewa kwenye moja ya vikao vya bunge la Jamhuri ya Muungano kutokana na msimamo wake juu ya mradi huo. 

Alisema tatizo la serikali imekuwa haitaki kufuata sheria  inayotaka ushirikishwaji wa wananchi kila hatua katika sera ya mipango miji. Pia aliongezea kusema wananchi wanataka majibu kuhusu lini mradi utaanza, wapi utaanzia, nini hatma yao hasa kuhusu fidia. 

Alipoulizwa swali na mmoja wa wanakigamboni kuhusu mgogoro  uliojitokeza baina yake na madiwani wa jimbo lake uliosababishwa na wao kutembelea moja vikao vya bunge kwa mualiko wa waziri wa ardhi na makazi Mhe Anna Tibaijuka, Ndugulile alijibu kuwa kwa sasa umeisha na kila mmoja ameshajua kosa lake.
 Mheshimiwa Faustine Ndugulile na Fina Mango baada ya kipindi cha Makutano, Magic FM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Asante sana Mhe.Faustin Ndugulile kwa msimamo wako!

    Nikiwa kama Mwananchi wa Jimbo lako la Ubunge ninakuunga mkono kwa hoja hizi:

    1.Ni utamaduni mbaya sana umejengeka nchini wa kutoshirikisha watu wananchi wa kawaida ktk masuala mbali mbali, mbaya zaidi unakuta kitu kinajiri eneo lao huku wakiwa hawapewi nafasi yeyote ktk maamuzi yake.

    2.Ni janga kubwa sana nchini Tanzania (nadhani Dunia nzima ni pekee hii inafanyika) nchi ina watu zaidi ya 45 Milioni lakini mambo mengi yanakuwa yanajulikana na yanaamuliwa na watu wasiozidi 45 tu !

    3.Maajabu ya Mussa yanakuja ikitokea mambo kwenda mrama ndio umuhimu wa Wananchi wa kawaida unaonekana huku wakibwagiwa maiti mikononi.

    4.Haya makundi yanayohodhi uwakilishi wa mambo na kuwatenga watu walio wengi yanajiona kama wao ndio wanajua sana wakati unaweza kuwa na werevu lakini ukazidiwa na mtu wa kawaida sana ktk jamii !!!

    5.Kuwa na Mamlaka isichukuliwa kuwa unafahamu kila kitu ni muhimu kushirikiana kimawazo na kimaamuzi.

    Hayo mambo matano (5) na mengine ndiyo Kiongozi Mhe.Ndugulile ameyaona na ametoa msomamo wake ili mambo yarekebishwe na tupige hatua mbele!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...