Watanzania wanaoishi jijini New York na Vitongoji vyake wakiwamo wawakilishi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, jana Jumamosi, waliungana na Familia ya Bw. Emmanuel Alfred Swere na Bi. Doto na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, katika Ibada ya kumuaga Jesca Emmanuel (12) aliyefariki ghafla Jumapili iliyopita.
Ibada ya kumuaga Jesca ilifanyika Bergen Funeral Home na iliongozwa na Mchungaji Perucy Butiku. Mazishi ya Marehemu Jesca yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne katika kijiji cha Bumbombi- Tarime Tanzania.
Raha ya Milele Umpe Eee Bwana na Mwanga wa Milele Umuangazie Apumzike kwa Amani. Amina
| Mama mzazi wa Jesca Bi. Doto akilia kwa uchungu mara baada ya kuona mwili wa mtoto wake. |
Baba mzazi wa Jesca, Bw. Emmanuel akilia kwa uchungu mara baada ya kumwona mtoto wake, pembeni yake ni Shangazi wa Jesca, Bi. Rose
Mchungaji Perucy Butiku akiongoza Ibada ya kumuombea Marehemu Jesca Emmnauel na kuwafariji wazazi wake, ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwakumbusha waombolezaji kwamba kila mmoja wetu anasiku yake atakayoitwa na Mwenye-Enzi Mungu, kama alivyoitwa Mtoto Jesca, ni siku ambayo hakuna mtu aijuaye. Na kwa sababu hiyo akasisitiza umuhimu wa kujianda. Ibada ilifanyika siku ya Jumamosi Bergen Funeral Home jijini New York.
Mdogo wake Jesca, Catherine akiwa ameelemewa na majonzi mazito kwa kuondokewa na dadayake, Catherine aliwatia uchungu waombelezaji pale alipomuaga Dada yake kwa kutamka " Bye Jesca".
Brigedia Jenerali Maganga Mwambata Jeshi katika Ubalozi wa Tanzania nchi Marekani, akiaga. Brigedia Jenerali Maganga ni kati ya Maafisa wanne waliowakilisha wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi Tuvako Manongi akiungana na waombelezaji wengine kumuaga marehemu Jesca. Baada ya ratiba ya kuaga, Balozi Manongi aliwashukuru watanzania kwa ushirikiano, upendo na mshikamano mkubwa waliouonyesha wakati wote wa kipindi cha maombolezo ya msiba huo na akawasihi kuendeleza umoja huo
Bw. Emmanuel na Bi. Doto wakiwa na mtoto wao, muda mfupi kabla ya sanduku kufungwa
Sanduku lenye mwili wa Jesca tayari kwa Safari ya kwenda Bumbombi- Tarime Tanzania kwa Mazishi.


Wapendwa wazazi Mungu awatie nguvu na faraja yake ijae mioyoni mwenu. Ni ngumu sana mnapomzika mtoto wenu tena kwa umri mdogo. Nasi tuliondokewa na mtoto mdogo ila faraj ya Mungu pekee ndio imetusimamisha tena. Poleni tena wazazi na familia yote
ReplyDeleteNodla
Poleni sana sana jamani kwani hata mie imenitoa machozi kwa kifo cha mtoto Mpendwa wenu. RIP Jesca
ReplyDeleteTunawapo Pole wazazi wa marehemu na familia yote kwa ujumla,pia salamu za pole kwa ndugu jamaa marafiki, na watanzania wote kwa ujumla.
ReplyDeleteMungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu
Poleni sana wafiwa wote. Mungu awape faraja. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake libarikiwe.
ReplyDeletePoleni sana wazazi wenzetu kwa kuondokewa na binti yenu mliyempenda Jesca.
ReplyDelete;Lakini ndugu hatutaki msijue habari zao waliolala mauti msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini''
Jesca hajafa amelala katika kristo naye tutaonana naye paradiso.
Mungu awatie nguvu sana na kuwafa faraja wakati wote wa huzini kubwa mioyoni mwenu.
Poleni sana.
Poleni sana wazazi, ndugu na marafiki... Inatia huzuni sana kupoteza mtoto mdogo hivyo.. Mungu ailaze roho ya Jesca mahala pema peponi... Amina
ReplyDelete
ReplyDeleteMungu awatangulie na kuwapa amani na faraja yake.
Napenda kutoa pole zangu kwa moyo mkunjufu kabisa.
ReplyDeletemimi siwafaham nyinyi ndugu zangu mlioko Nee York.
lakni napenda kuwajulisha tuko wote,katika kipindi hiki kwa sala na majonzi.Mungu atawapa nguvu.
Imeniuma sana kama,simfaham Jesca lakni ni mtoto mdogo kutangulia mbele za haki pamoja kufa hakubagui.
Mungu awape nguvu,nawaombea na namwombea Jesca alale salama.
Poleni sana wazazi! Poleni sana! I am just wordless
ReplyDeletePoleni sana Wazazi, Catherine, na familia yote. Mungu awape nguvu ya pekee katika kipindi hiki kigumu. Na amlaze Jesca wetu mpenzi mahali pema peponi amina.
ReplyDelete