Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii ( SSRA) imeendesha semina kwa baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Semina hiyo ililenga kuelimisha wajumbe juu ya masuala ya hifadhi ya Jamii nchini na majukumu ya Mamlaka (SSRA).
Akiwasilisha mada katika semina hiyo Mkurugenzi wa utekelezaji na uandikishaji Bi. Lightness Mauki aliwaeleza wajumbe juu ya mfumo wa hifadhi ya jamii Tanzania kuwa kuna aina nne za mifuko ya hifadhi ya jamii Tanzania, ambayo ni Mifuko ya Pensheni ( NSSF, PPF, PSPF, LAPF), mifuko ya akiba (GEPF),Mfuko wa Bima ya afya (NHIF/CHF) na mifuko ya hiari ambayo inaendeshwa na baadhi ya mashirika , makampuni na mifuko ya hifadhi ya Jamii kama PPF-DAS, GEPF-VSRS, NSSF & LAPF.
Pia aliwaeleza wajumbe juu ya majukumu ya Mamlaka likiwapo jukumu ya kulinda na kutetea maslai ya wanachama, hivyo wakati wote Mamlaka itahakikisha kuwa huduma za hifadhi ya Jamii ni bora na endelevu na zinaendeshwa kwa manufaa ya wanachama wake .
Mkurugenzi wa utekelezaji na uandikishaji Bi. Lightness Mauki akiwasilisha mada
Katbu mkuu ofisi ya raisi menejimenti ya utumishi wa Umma Bw. George Yambesi (kati) akisikiliza mada na viongozi wengine
Wajumbe wa baraza
Wajumbe wa bara- za wakisikiliza mada
Mkaguzi wa ndani SSRA- bw. Peter Mbelwa akinakili maswali na maoni wakati wa semina hiyo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...