Enzi hizo kulikuwa na mtindo wa Bumping ambao ulitamba sana. Na wakati huo huo Radio Tanzania Dar es salaam (RTD) katika idhaa ya nje yaani 'External Service' kulikuwa na kipindi maarufu cha kuomba nyimbo na kutumiana salamu cha 'At your request' kikiendeshwa na kaka Abdul Mtullya (Siku hizi yuko Ujerumani idhaa ya Kiswahili ya DW) na wimbo huu wa Carl Douglas wa 'Kung Fu Fighting' ulikuwa haukosi kuombwa....Wenye data zaidi kazi kwenu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ankal Michuzi,
    Tunashukuru kwa kutumbusha wimbo huu wa "Kung Fu Fighting" ulioimbwa na Carl Douglas,Enzi zile za Bumping,kwanza kucheza Bumping ilikuwa sharti uvae pamba za ki-bumping yaano bugalow au pekosi lenye upana wa inchi 18 chini,shati la kubana slimfit,duh ! viatu viwe ngazi 3 raizon,nywele lazima lazima zisimame afro,kwa akina mama wigi,enzi zile wavulana hawasuki nywele.
    Kwa sasa amini au usiamini mwanamuziki Carl Douglas baada ya maisha kumshinda kule USA ,alienda kwao jamaika, na kule jamaika maisha yaka magumu,yaani kama alivyoimba KUNG FU FIGHTING na maisha yapo hivi hivi ! Carl Douglas anaishi maisha ya kawaida
    katika mji wa HAMBURG,UJERUMANI.
    Mkongwe wa matangazo Mzee Abdul Mtullya yeye bado gado anaunguluma na Radio DW kiswahili Bonn.
    wadau
    FFU ughaibuni

    ReplyDelete
  2. Hicho kipindi kilikuwa kinaitwa "from me to you" kilikuwa kila jumapili saa 6:00 hadi 6:30 mchana........... na hiyo jumapili ilkuwa iko namna yake michuzi kwa dsm wakati huo lakini yamepita hayo........ always old is gold

    ReplyDelete
  3. Mataruma says:
    Alaaaa! kumbe ndio maana tulikuwa hatukuoni kwenye Mundo na Sikinde!!!

    ReplyDelete
  4. Zamani ilikuwa raha sana!

    Kwa kuvaa Raizoni, Bugaloo na Shati la Slim fit huku ukijua kucheza Bumping tayari Demu, tena Mademu umewapata kibaooo tena usione ajabu ukawa upo Jukwaani ukiendelea kuyarudi magoma huko kwenye viti unagombewa na Wanawake!

    Dahhh zamani kulikuwa kutamu, hivi ni nani Mwanasayansi Duniani anaweza kuurudisha mkanda tukarudi miaka ya 1970?

    ReplyDelete
  5. Kipindi hicho watu walikuwa wanakoga peku peku hakukuwa na mabalaa ya vitu kama 'miwaya' na maisha ya gharama za juu hadi sasa unakuta vitu kama penzi ukiliingia bila akili nzuri ni mawili yanakufika, looo 1.unafilisika au 2.unaondoka Duniani ukiwa na uzito wa Robo Kilo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...