Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Irene Isaka akiwasilisha maada kuhusiana na sekta ya Hifadhi ya Jamii Tanzania. Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA ), leo hii imeendesha semina kwa Wafanyakazi Wa Bodi ya Mishahara na Maslahi Katika Utumishi wa Umma. Semina hiyo imelenga katika kuelimisha wafanyakazi Wa Bodi ya Mishahara na Maslahi Katika Utumishi wa Umma juu ya masuala mbali mbali ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii na haswa majukumu ya Mamlaka .Semina hiyo ya siku mbili imehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka katika mifuko yote ya hifadhi ya Jamii Tanzania Bara , Wawakilishi kutoka wa Shirika la Nyumba ya Taifa ( NHC ), Wafanyakazi wa Bodi ya Mishahara na wawakilishi kutoka mfuko wa Bima ya Afya
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na uandikishaji Bi. Lightness Mauki akiwasilisha mada kuhusiana na Shughuli na majukumu ya SSRA
Mdau kutoka NSSF Mr. C. Magori akiuliza swali na kutoa ushauri kuhusiana na majukumu ya Bodi ya Mikopo
Katibu Mtendaji Wa Bodi ya Mishahara na Maslahi Katika Utumishi wa Umma Bi. Tamika Mwakahesya akiwasilisha mada kuhusiana na majukumu mbalimbali ya Bodi ya Mishahara
Mdau kutoka NHIF akielezea majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...