Stamina akiwachombeza kwa staili mashabiki.
Nyuso za burudani zilizokuwa zimefurika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
WASANII wa nguvu nchini wakiwemo Fid Q, Rich Mavoko, Dullayo, Kala Jeremiah, Stamina, bendi ya ‘Twanga Pepeta’, na mchuano wa wasanii wa muziki wa kufoka wa The Mic King waliwapagawisha maelfu ya wapenzi wa burudani waliofika katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live huko Mbagala jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.















ankal picha nyingine zinachafua hali ya hewa, hazina tofauti na kuandika neno baya,Zinajeruhi hisia za watu kwa kweli.
ReplyDeletemwisho wa siku hao wanenguaji wataamua kuonyesha namna ya kupigana mtanange jukwani
ReplyDeleteThere is artistic licence and there is artistic filth. Moja ya picha hapo juu ni ukesefu wa adabu tu, whatever you want to call it.
ReplyDeleteWe Ankal ni wewe mwenyewe umetuambia humu kuwa TUSICHAFUE HALI YA HEWA xaxa wewe mwenyewe mbona UMECHAFUA HALI YA HEWA humu hapo kwenye hiyo picha ya 8 toka juu bana?!
ReplyDeleteSheria msumeno hata kwako mwenye bana!
Hawa ndio wanafunzi wetu wa elimu ya juu, Tanzania, halafu unashangaa kwa nini wasomi wetu pamoja na degree walizonazo ni mbumbumbumbu wa kutupa. Ndugu zangu neno la Mungu halitanguki,Mungu akisema amesema, ameshasema kumcha(kumhofu Mungu) Bwana ni chanzo cha maarifa, Mithali 9:10. Kama unamcha Mungu huwezi ukashiriki mambo machafu tunayoyaona katika picha hizi na hapo ndipo unapoweza kupata msaada wa Mungu kukuwezesha kuwa na hekima na maarifa ya kipekee.Bado neema ipo tumkimbilie Bwana YESU, kabla ya hasira ya Mungu haijaachiliwa kwa Dunia,wakati huo Mungu hatakuwa na huruma tena. Kama unataka kupona na na hasira hii ya Mungu kwa watenda dhambi wote, fuatisha maneno, Bwana Yesu, nisamehe mimi mwenye dhambi,lifute jina langu katika vitabu vya hukumu andika jina langu katika kitabu cha uzima,naomba uwezo wa kushinda dhambi na ulimwengu, katika JINA LA YESU, AMEN.
ReplyDeleteHongera kwa uamuzi, huu ili kukaa katika usafi na utakatifu unahitaji kukaa katika mafundisho ya neno la Mungu, tafuta mahali popote ambapo watu wanajifunza neno la Mungu na kuliishi.
Mungu akubariki